"Thierry Henry ndiye pekee anaelewa hisia ya kufunga mabao mengi" - Erling Halaand

Halaand alifunga mabao matano katika mechi moja usiku wa Jumatano wakati Man City waliwakaribisha RB Leipzing uwanjani Etihad.

Muhtasari

• Mancity walijiunga na Chelsea kutoka Uingereza kutinga robo fainali ya kombe hilo la kilau bingwa Ulaya ambapo wanasaka kulinyanyua kwa mara ya kwanza katika historia ya kilabu hiyo.

Halaand amtambua Henry katika ufungaji mabao mengi.
Halaand amtambua Henry katika ufungaji mabao mengi.
Image: Facebook

Usiku wa Jumatani ulikuwa usiku wa historia kwa mshambulizi wa Manchester City Earling Halaand, baada ya kuisaidia timu yake kutinga robo fainali ya kombe la kilabu bingwa Ulaya kwa kuichabanga RB Leipzing.

City waliilemea Leipzing kwa kibano cha mabao 7 kwa nunge katika uga wa nyumbani Etihad, na kufanya idadi hiyo kuwa mabao manane kapa ukijumuisha ushindi wa bao moja kwa nunge katika mkumbo wa kwanza.

Katika karamu hiyo ya mabao, Halaand alifunga mabao 5 chini ya dakika 60 akiwa uwanjani.

Baada ya mchezo, Haaland alipata heshima ya kuhojiwa na watu watatu mashuhuri, Thierry Henry, Jamie Carragher, na Micah Richards, ambao walikuwa kwenye jukumu la uchambuzi wa Michezo ya CBS.

Aliulizwa jinsi alivyohisi kufunga mabao matano na hakuweza kujizuia kuwalenga mikuki Micah na Carragher huku akimpongeza Henry.

“Ni hisia nzuri sana na nafikiri wewe (Henry) ndiye mtu pekee unaelewa hisia ya kufunga mabao mengi. Kusema kweli hisia kama hiyo ni nzuri sana kwa sababu si rahisi kwa timu kufunga mabao 7 katika mchezo wa klub bingwa Ulaya,” Halaand alisema huku vicheko vikitanda katika meza hiyo ya wanahabari.

Mchezaji huyo hata hivyo alisisitiza kwamba angefunga mabao mengo haswa katika kipindi cha kwanza, akirejelea kumbukizi za nafasi za wazi alizozipoteza ambazo alikuwa katika nafasi nzuri ya kutia mpira wavuni.