Hali ya kutia huruma mcheza aliyegeuka kichaa akichakura mapipa ya taka kutafuta chakula

mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alitoweka kutoka klabuni na baadae akapatikana anaishi mfunguni mwa daraja moja, huku chakula chake kikiwa cha jalala.

Muhtasari

• Mchezaji huyo amekuwa akitoweka mara kwa mara kutoka nyumbani na kutafutwa kuwekwa chini ya ulinzi wa familia.

• Wiki jana aliripotiwa kutoweka na baadae picha zake zikasambaa akila chakula cha jalalani.

Khayelihle Shozi , mchezaji wa zamani wa Mamelod Sundowns.
Khayelihle Shozi , mchezaji wa zamani wa Mamelod Sundowns.
Image: Twitter,

Hisia mseto zimeibuliwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha kadhaa kusambazwa zikimuonesha aliyekuwa mchezaji maarufu wa soka Afrika Kusini akiwa kama kichaa wa kula kutoka kwa mapipa ya jalalani.

Kituo cha redio ya jamii, nchini humo, kilifichua kwenye ukurasa wao wa Facebook mnamo Alhamisi, Machi 16 kwamba nyota wa zamani wa Masandawana Khayelihle Shozi, ambaye hivi karibuni alionekana hana makazi, amepatikana na kuunganishwa na familia yake. .

“Shozi mwenye shida Amepatikana! Khayelihle Shozi, ambaye wiki iliyopita alionekana akizurura katika mitaa ya Vereeniging amepatikana na ameungana na familia yake huko Pinetown, KwaZulu-Natal. Theta FM inapenda kuwashukuru wote walioshiriki na kusaidia kupatikana kwake,” ilisomeka taarifa hiyo.

 Baada ya picha zake akiwa katika hali duni akichokora pipa la taka kwa chakula kuenezwa, watu mitandaoni walichukizwa na kitendo hicho, baadhi wakisema alikuwa na matatizo ya akili.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alipitia Katika timu za vijana ya Mamelod Sundowns na kupandishwa hadi timu ya wakubwa, Baadaye alipelekwa kwa mkopo Katika Vilabu vya SuperSport United, Black Leopard, TS Galaxy na Richard Bays.

 

Jarida la Zimoja lilifichua kuwa maisha ya Khayelihle Shozi yalibadilika na kuwa mabaya zaidi mnamo 2022 alipotoweka mara mbili katika klabu yake ya zamani ya soka ya Mamelodi Sundowns.

Klabu yake ya zamani ya Mamelodi Sundowns pia ilijitolea kuingilia kati katika mapambano yake na afya ya akili wakati huo.