Kylian Mbappé ateuliwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Ufaransa

Mchezo wake wa kwanza kama nahodha utakuwa wa Ijumaa wa kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Uholanzi nyumbani.

Muhtasari

• Mlinda mlango wa Tottenham Lloris alimaliza soka lake la kimataifa mwezi Januari baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Dunia mwezi mmoja mapema.

• Mbappe, ambaye ameichezea nchi yake mara 66, amekuwa akihusishwa pakubwa na jukumu hilo.

Mbappe ateuliwa nahodha mpya wa Ufaransa
Mbappe ateuliwa nahodha mpya wa Ufaransa
Image: Instagram

Kylian Mbappe amemrithi Hugo Lloris aliyestaafu kama nahodha wa Ufaransa, chanzo cha karibu cha timu hiyo kiliiambia AFP siku ya Jumatatu.

Mshambulizi huyo wa Paris Saint-Germain Mbappe, 24, alikubali pendekezo hilo baada ya mazungumzo na kocha Didier Deschamps mapema siku hiyo, kulingana na ripoti ya kila siku ya michezo ya Ufaransa L'Equipe.

Mlinda mlango wa Tottenham Lloris alimaliza soka lake la kimataifa mwezi Januari baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Dunia mwezi mmoja mapema.

Lloris, 36, alikuwa nahodha kwa zaidi ya muongo mmoja.

Mshambulizi wa Atletico Madrid Antoine Griezmann alitangazwa kuwa makamu wa nahodha baada ya beki wa kati wa Manchester United Raphael Varane pia kutundika daruga zake kufuatia kushindwa na Argentina mwezi Desemba.

Mbappe, ambaye ameichezea nchi yake mara 66, amekuwa akihusishwa pakubwa na jukumu hilo kwa wiki kadhaa na alifunga hat-trick katika kupoteza fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuisaidia Les Bleus kutwaa ubingwa mwaka wa 2018.

Mshambulizi huyo wa zamani wa Monaco ni makamu nahodha wa PSG nyuma ya Marquinhos wa Brazil na aliongoza timu hiyo wakati wa kukosekana kwa beki huyo Jumapili walipolazwa na wageni Rennes.

Mchezo wake wa kwanza kama nahodha utakuwa wa Ijumaa wa kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Uholanzi kwenye Uwanja wa Stade de France.

Alipoulizwa ni nani anaamini anafaa kuwa nahodha ajaye wa Ufaransa, Lloris aliiambia Telefoot, "Kuna mchezaji mmoja ambaye anakuwa na nguvu zaidi katika kila nyanja ndani na nje ya uwanja na hata katika utendakazi wa chumba cha kubadilishia nguo - ni Kylian Mbappe." Ikiwa hii haitoshi, Mbappe amepokea uteuzi mwingine mkubwa katika vita vya kuwa nahodha mpya wa Ufaransa.