Nyota wa Chelsea, ManCity, Man-U wafuatiliwa zaidi TikTok, Arsenal wakosa kwenye 10 bora

Orodha hiyo ilitawalwa pakubwa na wachezaji wa City, United, Chelsea na Tottenham, huku mastaa wa Arsenal wakikosekana.

Muhtasari

• Earling Halaand si tu anaongoza katika ufungaji wa mabao bali pia katika kutazamwa TikTok.

• Licha ya Arsenal kuwa na mastaa wengi wanaofanya vizuri, hakuna hata mmoja aliyeingia kwenye 10 bora.

Wachezaji walioongoza katika ufuatiliwa pakubwa TikTok.
Wachezaji walioongoza katika ufuatiliwa pakubwa TikTok.
Image: Instagram

Mtandao wa klipu fupi fupi wa TikTok ambao hauna muda mrefu kwenye soko la kidijitali umefanya rahisi kwa  nyota wa Sanaa mbalimbali kujulikana na kujumuika na mashabiki wao.

Wacheza kandanda mara nyingi hujulikana kwa umahiri wao uwanjani. Lakini pia ujio wa TikTok umewafanya baadhi kutamba kwa kupakia nyakati zao nzuri uwanjani na kuwafurahisha mashabiki wao ndani na nje ya uwanja.

Na ufuasi wa wachezaji wengi katika kizazi hiki cha dijitali umeendelea kuongezeka hata Zaidi kwani wengi sasa wamekumbatia mtandao wa TikTok kama njia moja ya kuwafikia mashabiki zao.

Top Rated Casinos ilizamia suala hili na kutoa orodha ya wachezaji nyota wa ligi kuu ya premia, EPL ambao wana ufuasi mkubwa kwenye mtandao wa TikTok, orodha hii ikionesha wachezaji ambao wanatazamwa sana pindi wanapofanya vipindi vya moja kwa moja au kupakia video zao kwenye mtandao huo.

Mshambuliaji wa Manchester City Earling Braut Halaand sit u anaongoza katika orodha ya ufungaji mabao kwenye ligi hiyo bora Zaidi duniani, lakini pia kwenye mtandao wa TikTok, mchezaji huyo ndiye anaongoza kwa wachezaji waliotazamwa Zaidi.

Halaand ana watazamaji bilioni 4.1 huku akifuatiliwa na kiungo wa kati wa Manchester United, Casemiro.

Orodha hiyo ya nyota kumi bora waliotazamwa Zaidi TikTok imetawalwa kwa kiasi kikubwa na wachezaji kutoka timu za Manchester United, Manchester City, Chelsea na Tottenhma, huku Arsenal ambayo ni moja ya timu kubwa ikiwa haina staa wao hata mmoja kwenye orodha hiyo.

Hii hapa orodha kamili kwa hisani ya TopRatedCasinos.

1 Erling Haaland wa Manchester City na bilioni 4.1

2 Casemiro wa Manchester United  na bilioni 3.6

3 Mason Mount wa Chelsea na bilioni 3  

4 Son Heung-min wa Tottenham na bilioni 2.9

5 Bruno Fernandes wa Manchester United na bilioni 2.8

6 Kai Havertz wa Chelsea na bilioni 2.2

7 Jack Grealish wa Manchester City na bilioni 2.1

8 Phil Foden wa Manchester City na bilioni 1.9

9 Kevin De Bruyne wa Manchester City na bilioni 1.8

10 Harry Kane wa Tottenham na bilioni 1.5