logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bayern Munich yamsimamisha Sadio Mane na kumtoza faini kwa 'kumpiga' mchezaji mwezake

"Sane na Mane walionekana uwanjani wakizozana katika hatua za mwisho za mechi hiyo

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 April 2023 - 15:49

Muhtasari


  • Mane pia atapigwa faini na hatakuwa sehemu ya kikosi cha Bayern kwa ajili ya mchezo wao wa nyumbani wa Bundesliga dhidi ya Hoffenheim Jumamosi.

Bayern Munich imemsimamisha Sadio Mane baada ya kumpiga usoni mchezaji mwenza Leroy Sane kufuatia kichapo cha Jumanne cha Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City.

Mane pia atapigwa faini na hatakuwa sehemu ya kikosi cha Bayern kwa ajili ya mchezo wao wa nyumbani wa Bundesliga dhidi ya Hoffenheim Jumamosi.

Sky Germany iliripoti kuwa mdomo wa Sane ulikuwa ukivuja damu baada ya ugomvi huo na wachezaji hao wawili walihitaji kutenganishwa na wenzao kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Taarifa kutoka Bayern ilisema: "Sadio Mane, 31, hatakuwepo kwenye kikosi cha FC Bayern kitakachocheza nyumbani dhidi ya 1899 Hoffenheim Jumamosi ijayo.

Sababu ni utovu wa nidhamu wa Mane baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa FC Bayern dhidi ya Manchester City.

Aidha, Mane atatoa faini.

"Sane na Mane walionekana uwanjani wakizozana katika hatua za mwisho za mechi hiyo Jumanne usiku, ambapo City waliwafunga mabingwa hao wa Ujerumani mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Etihad katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved