Sadio Mané ampiga ngumi Leroy Sané mdomoni baada ya Bayern kushindwa na ManCity

Inaarifiwa kwamba Mane alighadhabishwa na kitendo cha Sane kukosa nafasi za wazi dhidi ya timu yake ya zamani Manchester City.

Muhtasari

• Hata hivyo, uongozi wa timu ya Bayern hawajatoa maoni yoyote kuhusu tukio hilo.

• Mane anadaiwa kumpiga ngumi mdomoni Sane na ilibidi wametenganishwa huku Sane akibaki na jeraha kwenye midomo yake.

Sadio Mane adaiwa kumpiga ngumi mdomoni Leroy Sane.
Sadio Mane adaiwa kumpiga ngumi mdomoni Leroy Sane.
Image: Twitter

Taarifa kutoka kambi ya Bayern Munich ni kwamba baada ya kipigo mikononi mwa Manchester City usiku wa Jumanne ugani Etihad, joto liliibuka kambini na wachezaji kurushiana mangumi kwa kulaumiana kufuatia kipigo hicho.

Nyota wa Bayern Munich walilazimika kuwatenganisha Sadio Mane na Leroy Sane aliyejeruhiwa ndani ya chumba cha kubadilishia nguo baada ya kutokea ugomvi kufuatia kushindwa na Manchester City.

Mabingwa hao wa Bundesliga wanakabiliwa na kibarua cha kupindua kipigo cha mabao matatu kwa nunge katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa na mawinga hao wakaambulia kipigo kwa muda wote.

Sane na Mane walionekana wakikabiliana walipokuwa wakitoka nje ya uwanja kwenye Uwanja wa Etihad na mzozo ulizidi kupamba moto waliposhuka kwenye handaki.

Mane alikasirishwa na jinsi Sane alivyozungumza naye wakati wa mabishano na inaaminika kuwa alimpiga usoni mchezaji huyo wa zamani wa City.

Sane - ambaye alikuwa tishio kubwa la Bayern usiku huo - aliachwa na mdomo ukiwa na damu kabla ya kuvutwa kutoka kwa kila mmoja wao.

Mane inasemekana alichukuliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Munich kwa gari la kibinafsi wakati timu hiyo iliporejea Jumatano, wakati Sane alipanda gari la timu hiyo.

Tukio hilo linaonyesha kazi kubwa iliyo mikononi mwa Thomas Tuchel ikiwa Bayern wanataka kuzindua mchezo wa marudiano wiki ijayo kwenye Uwanja wa Allianz Arena.

Hata hivyo, uongozi wa timu ya Bayern hawajatoa maoni yoyote kuhusu tukio hilo.

Mabingwa hao watetezi wa Ujerumani waliadhibiwa kikatili na Manchester City katika mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.