Ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji wa Arsenal kutoka yashika moto kabla ya kupaa

Kisa hicho kilitokea baada ya ndege mnyama kuruka ndani ya injini ya ndege hiyo na kusababisha kishindo kikubwa na moto.

Muhtasari

• Taarifa hiyo ilisema: ''Ndege yetu ilitengeneza tatizo la kiufundi kabla ya kupaa nchini Ujerumani Jumapili jioni."

Ndege ya timu ya Arsenali ilishika moto
Ndege ya timu ya Arsenali ilishika moto
Image: Twitter

Ndege iliyokuwa imebeba timu ya wanawake ya Arsenal ikirejea kutoka kwa mechi ya nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Wolfsburg iliwaka moto kwenye njia ya kurukia ndege Jumapili jioni.

Kisa hicho kilitokea katika uwanja wa ndege wa Braunschweig Wolfsburg baada ya ndege mnyama kuruka ndani ya injini muda mfupi kabla ya kuruka na kusababisha kishindo kikubwa.

Mara moja miale ilianza kutoka kwenye injini ya kushoto ya Boeing 737, na marubani waliokuwa ndani ya ndege hiyo wakawahamisha haraka abiria, kikiwemo kikosi cha kwanza cha Arsenal, hadi mahali pa usalama.

Arsenal walitoa taarifa kuthibitisha kuwa wamerejea nyumbani salama Jumatatu asubuhi.

Taarifa hiyo ilisema: ''Ndege yetu ilitengeneza tatizo la kiufundi kabla ya kupaa nchini Ujerumani Jumapili jioni."

'Kutokana na hayo, tulibaki Wolfsburg usiku kucha Jumapili kabla ya kuruka kurudi Uingereza Jumatatu mchana. Tungependa kuwashukuru wafanyakazi walio ndani ya ndege na walio chini kwenye uwanja wa ndege kwa usaidizi wao.'

Timu hiyo ilitumia shirika la ndege la Malta kuruka hadi Ujerumani siku ya Jumamosi, na ilitakiwa kurejea na shirika lile lile jioni iliyofuata.

Hata hivyo, baada ya injini kushika moto, walilazimika kubadili shirika la ndege badala ya kurejea Uingereza Jumatatu asubuhi.

Kufuatia kurejea kwao kutoka Ujerumani, Arsenal sasa wanaweza kutazamia kujaribu kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka huu baada ya kupambana na kupata sare ya 2-2 katika mechi ya kwanza ya Jumapili.