Afcon 2027: Kenya, Tanzania na Uganda zawasilisha maombi ya kuwa mwenyeji

Kenya ina uwanja mmoja tu ulioidhinishwa kwa michezo ya kimataifa na Caf,

Muhtasari
  • Hata hivyo, haijulikani ni kiasi gani cha uwekezaji kitahitajika kuruhusu aidha ya Botswana au ya pamoja ya Afrika Mashariki kufanikiwa.

Kenya, Tanzania na Uganda wanatazamiwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2027.

Majirani hao watatu wa Afrika Mashariki wamewasilisha ombi la pamoja la nia yao na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), bodi inayoongoza ambayo huandaa michuano hiyo inayofanyika kila baada ya miaka miwili.

Mataifa mengine matatu pia yamesajili nia - Algeria, Botswana na Misri.

Misri ilikuwa mwenyeji wa Afcon hivi majuzi 2019, wakati mapema mwaka huu Algeria ilikuwa mwenyeji wa Michuano ya Mataifa ya Afrika (Chan) - mashindano ya bara la Afrika kwa wachezaji wa ndani - ikimaanisha kuwa nchi hizo mbili haziwezi kuhangaika linapokuja suala la mahitaji ya miundombinu.

Hata hivyo, haijulikani ni kiasi gani cha uwekezaji kitahitajika kuruhusu aidha ya Botswana au ya pamoja ya Afrika Mashariki kufanikiwa.

Hadi wiki iliyopita, ombi la Botswana pia lilipaswa kuwa la pamoja, lakini Namibia ilijitoa dakika za mwisho, kwa sababu ya wasiwasi wa kifedha.

Kenya ina uwanja mmoja tu ulioidhinishwa kwa michezo ya kimataifa na Caf, Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo kaunti ya Nairobi.

Nchi hiyo ilipokonywa haki ya kuandaa Chan 2018 miezi minne tu kabla ya fainali hizo kwa sababu viwanja kadhaa havikuwa tayari.

Mnamo Desemba, serikali ya Kenya ilitoa taarifa kuhusu ombi lake tarajiwa la 2027 ikifichua kuwa baraza lake la mawaziri "liliidhinisha ufufuaji wa soka kama nguzo kuu ya tasnia ya kijamii ya taifa letu" katika jitihada za "kufufua matarajio ya soka ya Kenya".