Pep Guardiola amedai lifanyike gwaride la heshima kwa ajili ya wachezaji wake na wafanyakazi wa klabu hiyo kuadhimisha bao la rekodi Erling Haaland la Primia Ligi – kumuonyesha mshambuliaji huyo jinsi mafanikio aliyoyapata yalivyo maalumu.
Kufunga bao la 3 - 0 dhidi ya West Ham kwa Haaland kunamaanisha kuwa sasa ana mabao 35 ya ligi katika msimu.
Amevunja rekodi ambayo awali alimuweka katika kiwango sawa na Alan Shearer na Andy Cole.
"Wakati kuna tukio maalumu, tunapaswa kuonyesha ni kwa jinsi gani lilivyo maalumu," amesema Guardiola.
Wachezaji wenzake wa Manchester city, pamoja na Guardiola na wahudumu wengine wa klabu hiyo waliokuwa katika chumba cha mavazi, walijipanga mstari kumpatia heshima Haaland alipokuwa njiani kuelekea katika chumba cha kubadilisha mavazi.