Michael Olunga ashinda tuzo ya mfungaji bora katika ligi ya Qatar

Mabao manne ya Olunga yaisaidia timu ya Al Duahail kuibuka mabingwa wa ligi ya Qatar.

Muhtasari

• Mchezaji huyo wa timu ya Al-Duhail alifunga mabao manne katika mechi ya jumatatu dhidi ya Shamal Sc na kuisaidia timu yake kuibuka mabingwa wa ligi hio.

• Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Kenya alinyakua taji yake ya pili msimu huu baada ya kuongoza Al Duhail kwa kufunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza na kuongeza nyingine pindi tu kipindi cha pili kilipoanza.

Michael Olunga atuzwa kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka kama mfungaji bora wa ligi ya Qatar
Michael Olunga atuzwa kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka kama mfungaji bora wa ligi ya Qatar
Image: TWITTER

Mshambulizi wa timu ya taifa ya Kenya Michael Olunga ndiye mfungaji bora wa ligi ya taifa nchini Qatar.

Mchezaji huyo wa timu ya Al-Duhail alifunga mabao manne katika mechi ya jumatatu dhidi ya Shamal Sc na kuisaidia timu yake kuibuka mabingwa wa ligi hiyo.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Kenya alinyakua taji yake ya nne msimu huu baada ya kuongoza Al Duhail kwa kufunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza na kuongeza lingine pindi tu kipindi cha pili kilipoanza.

Al-Duhail wameongoza ligi hio ya timu 12 wakiwa na pointi 51 kutoka kwa mechi 22, pointi mbili juu ya mpinzani wao wakaribu Al-Arabi, ambao waliwazaba Al-Sadd 2-1 katika mechi nyingine muhimu iliyochezwa Jumatatu jioni.

Ni mara ya kwanza kwa Olunga kushinda taji la Ligi ya Qatar Stars akiwa na Al-Duhail tangu ahamie yimu hio mwaka wa 2021.

Kwa mabao hayo manne, nahodha huyo wa Harambee Stars alitwaa kiatu cha dhahabu msimu huu kwa mabao 22. Hii ni mara ya pili ya mshambulizi huyo kutatawazwa kama mfungaji bora. Msimu uliopita pia aliweza kupea kiatu hicha cha dhahabu baada ya kuitia nyavuni mabao 24.