Solskjaer: Alex Ferguson aliniomba radhi baada ya kunikejeli kumweka CR7 benchi

Video iliibuka mwaka 2021 ikionyesha Ferguson akikejeli maamuzi ya Solskjaer kumweka Ronaldo benchi katika mechi ya United dhidi ya Everton.

Muhtasari

• Ferguson alisikika akikejeli Solskjaer kuwa angeweka wachezaji wake wa umahiri kwenye mechi hiyo na pengine angepata ushindi.

• Mechi hiyo iliishia sare licha ya Ronaldo kuingia dakika za 57 na alikuwa kwenye fomu nzuri wakati aliwekwa benchi.

Ole Gunnar Solskjaer adai Ferguson alimuomba msamaha baada ya kumkejeli kumweka Ronaldo benchi.
Ole Gunnar Solskjaer adai Ferguson alimuomba msamaha baada ya kumkejeli kumweka Ronaldo benchi.
Image: Twitter

Aliyekuwa kocha wa Man U, Ole Gunnar Solskjaer amefichua jinsi Sir Alex Ferguson aliomba msamaha baada ya kunaswa kwenye kamera akikosoa uamuzi wa meneja huyo raia wa Norway kumweka benchi Cristiano Ronaldo kwa sare ya Manchester United dhidi ya Everton mwaka 2021.

Kwa kushangaza Ronaldo alitajwa kama mbadala wa mechi ya United dhidi ya The Toffees licha ya kwamba alikuwa amefunga mabao matano katika mechi sita baada ya kurejea Old Trafford mapema mwakani.

Ronaldo aliingizwa uwanjani baada ya dakika 57 lakini hilo halikumzuia Ferguson kulaani uamuzi wa kiufundi wa Solskjaer alipokuwa akizungumza na gwiji wa UFC Khabib Nurmagomedov.

Ferguson alionekana akizungumza na mshambuliaji huyo wa Dagestani baada ya mechi ya Old Trafford na mada ya mchezo ilipoibuka, Mskoti huyo alisema: "Lakini pia nadhani (Everton) walipoona Ronaldo hachezi, ilikuwa kidogo. ...'

Khabib alijibu: 'Aliingia kipindi cha pili...' - lakini Ferguson alimkatiza gwiji huyo wa UFC na kusema: 'Najua, lakini unapaswa kuanza na wachezaji wako bora kila mara.'

Matamshi ya Ferguson yalienea na Solskjaer alilazimika kutetea uamuzi wake wa kumweka benchi Ronaldo katika mahojiano yake baada ya mechi - akisema: 'Unafanya maamuzi katika msimu mzima mrefu na lazima usimamie mzigo wa wachezaji. Uamuzi ulikuwa, kwangu, ndio sahihi leo'.

Solskjaer sasa amefichua kwamba Ferguson alimpigia simu muda mfupi baada ya video hiyo kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kuomba radhi kwa maoni yake - akidai alijua jinsi 'ilivyokuwa ngumu'.

Solskjaer aliliambia The Athletic: "Hiyo ndiyo mara moja Sir Alex amewahi kuniomba msamaha. Alinaswa kwenye video akisema, "Unapaswa kucheza wachezaji wako bora kila wakati," baada ya Ronaldo kuanza kwenye benchi kwa mchezo mmoja.

'Yeye (Ferguson) alinipigia simu na kuniomba msamaha kwa sababu anajua jinsi ilivyo ngumu.'

Solskjaer alifukuzwa kazi kama Manchester United mnamo Novemba 2021 baada ya kichapo cha 4-1 kutoka kwa Watford kuendeleza matokeo mabaya.

Alikuwa amepoteza mechi saba kati ya 13 za mwisho akiwa kocha, na kuilazimu klabu kuchukua hatua na kumwondolea majukumu yake.