Chelsea kumteua Pochettino kama meneja wao wa msimu 2023/2024

Pochettino alikuwa mkufunzi wa timu ya PSG na Timu ya Southampton.

Muhtasari

• Kocha huyo pia alikua mkufunzi wa timu ya PSG katika ligi kuu ya nchini ya Ufaransa na timu ya Southampton.

• Meneja huyo mwenye umri wa miaka 51 atamrithi mchezaji wa zamani wat imu hiyo ya Chelsea Frank Lampard.

Kocha Mauricio Pochettino
Gatty Images Kocha Mauricio Pochettino
Image: BBC Sport

Klabu ya Chelsea inaripotiwa kumwinda meneja wa zamani wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino kuwa kocha wao wa msimu ujao.

Kocha huyo pia alikua mkufunzi wa timu ya PSG katika ligi kuu ya nchini ya Ufaransa na timu ya Southampton.

Tetesi hizi zilithibitishwa na mwanahabari tajika wa masauala ya uhamisho wa wachezaji Fabrizio Romano.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 51 atamrithi mchezaji wa zamani wa timu hiyo ya Chelsea Frank Lampard.

Jukumu la Frank Lampard kama meneja wa muda litakamilika mwishoni mwa msimu huu.

Lampard alichukua hatumu kutoka kwa Graham Potter baada ya Potter kufutwa kazi mwanzoni mwa Aprili baada ya kuifunza klabu hiyo kwa chini ya miezi saba.

Klabu hiyo Licha ya kutumia pauni milioni 600 katika madirisha ya mwisho ya uhamisho inashikilia namba ya 11 baada ya mechi 35 katika ligi kuu nchini Uingereza.

Klabu hiyo pia haitacheza mashindano yoyote ya ulaya msimu ujao.

Timu hiyo pia haitacheza mashindano ya Ulaya msimu ujao.