Thomas Partey avunja kimya kupoteza nafasi yake kwa Jorginho katika kikosi cha 1 Arsenal

Kumbuka kwamba naibu nahodha wa Ghana, ambaye alikuwa ameanza mechi 26 za ligi kwa The Gunners msimu huu, alibadilishwa na kiungo wa Kiitaliano Jorginho.

Muhtasari

• Partey alikiri kwa Standard Sports kwamba hakuwa na wasiwasi kuhusu kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza.

Partey avunja kimya kupoteza nafasi yake kikosini Arsenal
Partey avunja kimya kupoteza nafasi yake kikosini Arsenal
Image: Twitter

Kiungo wa kati wa Arsenal, Mghana Thomas Partey ametuma taarifa ya kuwaondoa hofu mashabiki wake baada ya kukosa kuanza kwa mechi tatu za awali za Arsenal za Ligi Kuu ya Uingereza.

Kumbuka kwamba naibu nahodha wa Ghana, ambaye alikuwa ameanza mechi 26 za ligi kwa The Gunners msimu huu, alibadilishwa na kiungo wa Kiitaliano Jorginho.

Partey alikiri kwa Standard Sports kwamba hakuwa na wasiwasi kuhusu kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza.

"Nina furaha sana kwake (Jorginho) kwa sababu, kwa wiki kadhaa, alikuwa bora kwenye mazoezi na kisha mwisho, unaona hivyo kwenye mchezo."

Partey aliendelea kusifu uchezaji mwenzake wa hivi majuzi na kuangazia umuhimu wa ushindani kwenye kikosi.

"Nina furaha sana kwake na pia ninafurahi kwamba kila mchezaji yuko tayari kuingilia, kwa hivyo hakuna anayeweza kulala. Nadhani ni nzuri na ninatumai kila mtu katika nafasi hiyo atakuwa tayari kuingilia pindi atakapopata nafasi. Madhumuni ya klabu ni kuunda ushindani na hiyo inasaidia klabu kukua zaidi, na pia inatusukuma kuweza kujitoa katika mchezo wetu bora.”

Wakati huo huo washika bunduki hao wako hatarini kuona taji la Ligi Kuu ya Uingereza likipita katika mchujo wao msimu huu, wakiwa wamesalia nyuma ya Manchester City wakiwa wamesalia na mechi mbili pekee.

Arsenal waliona matumaini yao yakiyeyuka nyumbani baada ya kichapo kikali kutoka kwa wageni Brighton usiku wa Jumapili ugani Emirates.

Partey avunja kimya kupoteza nafasi yake kikosini Arsenal
Partey avunja kimya kupoteza nafasi yake kikosini Arsenal
Image: Twitter