Mfanyabishara wa Qatari Sheikh Jassim afanya maboresho ya ofa kununua Man United

Dau jipya liliwasilishwa Jumanne asubuhi huku mazungumzo na Raine Group, wanaoshughulikia mauzo yakifanyika.

Muhtasari

•Mfanyabiashara huyo wa Qatar ambaye ni mwekezaji katika benki pamoja na Sir Jim Ratcliffe's Ineos Group ndizo pande mbili kuu zinazotazamia kuinunua klabu hiyo ya Old Trafford.

•Dau jipya  litalipa deni lote na kujumuisha pesa nyingine za kando ambazo zitaelekezwa moja kwa moja katika klabu na shughuli za kijamii za eneo.

Image: BBC

Mfanyabiashara maarufu wa Qatar Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani amefanya maboresho ya ofa yake ili aweze kuinunua klabu ya soka ya Manchester United.

Vyanzo vya habari vimeiambia BBC Sport kwamba dau jipya liliwasilishwa Jumanne asubuhi huku mazungumzo na Raine Group, wanaoshughulikia mauzo yakifanyika.

Mfanyabiashara huyo wa Qatar ambaye ni mwekezaji katika benki pamoja na Sir Jim Ratcliffe's Ineos Group ndizo pande mbili kuu zinazotazamia kuinunua klabu hiyo ya Old Trafford.

Makundi hayo yote mawili yaliwasilisha dau la tatu mwishoni mwa mwezi Aprili.

Inafahamika kuwa dau jipya ambalo ni kwa ajili ya kuinunua 100% ya klabu , litalipa deni lote na kujumuisha pesa nyingine za kando ambazo zitaelekezwa moja kwa moja katika klabu na shughuli za kijamii za eneo.

Takwimu za mwezi Machi zilionesha kuwa United walikuwa wanadaiwa deni la pauni milioni 969.6, likijumuisha deni la jumla, mikopo ya benki, na ada za kutuma pesa zinazohusiana na malipo.

Familia ya Glazer ilitangaza mwezi Novemba kuwa wanaangalia uwezekano wa kuiuzaManchester United huku waki "angalia mikakati mbadala".