Stori za jaba? Kipa Emiliano Martinez aapa kumleta Lionel Messi klabuni Aston Villa

"Messi ni mnywaji mwenza wangu, tunakula asados ​​[nyama choma] kila wiki. Nitapunguza mshahara wangu, tutajitahidi." - Martinez

Muhtasari

• Martinez, 30, na Messi, 35, walishinda Kombe la Dunia pamoja na Argentina nchini Qatar mwishoni mwa mwaka jana.

• Messi anatarajiwa kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu na kumekuwa na hati hati kuhusu klabu ambayo atatumikia msimu ujao.

Kipa wa Argentina aapa kumleta Lionel Messi Aston Villa
Kipa wa Argentina aapa kumleta Lionel Messi Aston Villa
Image: SUN//TWITTER

Mlinda mlango wa klabu ya Aston Villa Emi Martinez ametoa ofa nzuri ya kumleta Lionel Messi katika klabu hiyo.

Martinez, 30, na Messi, 35, walishinda Kombe la Dunia pamoja na Argentina nchini Qatar mwishoni mwa mwaka jana.

Messi alikuwa mfungaji bora wa pamoja nchini Qatar alipoiongoza nchi yake kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu.

Na Martinez alichukua jukumu muhimu katika ushindi huo kwani alikuwa shujaa katika mikwaju miwili ya penalti na kupokea Golden Glove kwa kipa bora.

Sasa Messi anakadiria chaguo lake anapojiandaa kufanya kile ambacho kinaweza kuwa hatua ya mwisho ya maisha yake ya klabu.

Anatarajiwa kuondoka Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu baada ya miaka miwili, baada ya kuzomewa na mashabiki wake mwezi uliopita.

Gwiji huyo wa Barcelona amekuwa akihusishwa na kutaka kurejea kwa wababe hao wa Catalonia, ingawa haijafahamika iwapo wataweza kumudu mshahara wake.

Messi pia ameripotiwa kupokea ofa nono ya pauni milioni 350 kwa mwaka kutoka kwa klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia.

Lakini Martinez amejitokeza na kujitolea kupunguza mshahara wake ili kumleta raia mwenzake Midlands.

Aliiambia ESPN: "Ikiwa wanampigia simu Messi, ningemleta hapa ... huko Villa. Haya, jamani, ni mnywaji mwenza wangu, tunakula asados ​​[nyama choma] kila wiki. Nitapunguza mshahara wangu, tutajitahidi."

Villa wako katika mstari wa kuwania nafasi ya kushiriki Ligi ya Europa Conference msimu ujao huku wakishika nafasi ya saba kwenye jedwali la Ligi ya Premia.

Lakini kuhamia kwa Messi kunasalia kuwa ndoto ya kupendeza wakati Muargentina huyo anakaribia hatua za mwisho za kazi yake.

Baada ya PSG kumpa adhabu ya kufungiwa kwa wiki mbili kwa kukosa mazoezi kutokana na safari ya kwenda Saudi Arabia, mashabiki wa mabingwa hao wa Ligue 1 walimzomea aliporejea dimbani.

Na uhusiano uliovunjika kati ya Messi na klabu hiyo umemaliza mjadala wowote kuhusu yeye kuongeza muda wake wa kukaa katika mji mkuu wa Ufaransa.