Kocha wa Taifa Engin Firat akitaja kikosi kitakachoshiriki mashindano Mauritius

Firat alisema kuwa alikuwa na wakati mgumu kuwachagua wachezaji hao kutoka kwa wachezaji wengi wenye kipaji kubwa.

Muhtasari

• Mturuki huyo alisema watatumia mchuano huo kujipima nguvu  kabla ya michuano ijayo ya kimataifa.

• Harambee stars wataanza mazoezi yao siku ya jumatatu na wanatarajiwa kuelekea Mauritius tarehe 10 Juni .

Kocha Mkuu wa Harambee Stars Engine Firat.
Kocha Mkuu wa Harambee Stars Engine Firat.
Image: Maktaba

Kocha mkuu wa Harambee Stars Engin Firat amekitaja  kikosi cha wachezaji 30  kabla ya mashindano ya Mataifa manne yanayotarajiwa kufanyika Juni 11-18 nchini Mauritius.

Firat alisema kuwa alikuwa na wakati mgumu kuwachagua wachezaji hao kutoka kwa wachezaji wengi wenye kipaji kubwa.

 "Kikosi hiki cha wachezaji 30 kinajumuisha nyota wanaocheza soka yao humu chini waliotolewa kwa kiasi kikubwa kutoka Ligi Kuu ya Kenya pamoja na wachezaji wa nchi za kigeni," Firat alisema alipokuwa akizindua kikosi hicho.

Mturuki huyo alisema watatumia mchuano huo kujipima nguvu  kabla ya michuano ijayo ya kimataifa.

"Nimechagua kikosi hiki ili kujiandaa kwa michuano yajayo ya CAF na FIFA. Zaidi ya hayo, shindano hili linawapa wachezaji wetu fursa ya kuonyesha kiwango chao."

Baadhi ya wachezaji wa humu nchini waliochaguliwa kwa mara ya kwanza kwenye timu ya taifa ni mlinzi Simon Masaka (Sofapaka), Kevin Luke Otiala (Kariobangi Sharks), Charles Ouma (Polisi wa Kenya), na Moses Shummah (Kakamega Homeboyz).

Harambee stars wataanza mazoezi yao siku ya jumatatu na wanatarajiwa kuelekea Mauritius tarehe 10 Juni .

Stars watachuana na timu ya taifa ya Mauritius, Pakistan na Djibouti.

Kikosi hicho kiliwajumuisha walinzi Ian Otieno( Zesko, Zambia), Bryne Odhiambo (KCB) ,Brian Bwire (Tusker), Simon Masaka   (Sofapaka).

Mabeki Joseph Okumu (Gent, Belgium), Daniel Anyembe (Viborg, Denmark), Eric Ouma (AIK, Sweden) Collins Shichenje (KUPS), Daniel Sakari (Tusker), David Ochieng (Kenya Police), Abud   Omar (Kenya Police), Mohamed Siraj (Bandari), Kevin Luke Otiala (Kariobangi Sharks), Robinson Kamura (Kakamega Homeboyz).

Viungo Amos Nondi (Ararat, Armenia), Richard Odada (Philadelphia Union, USA), Kenneth Muguna (Azam, Tanzania), Teddy Akumu (Sagan Tosu, Japan), Alvin Mangeni (Kenya Police), Clifton Miheso (Kenya Police), Charles Ouma (Kenya Police), Abdallah Hassan (Bandari), Joseph Mwangi (Nzoia Sugar), Alpha Onyango (Gor Mahia), Bonface Omondi- (Gor Mahia), Victor Omune  (AFC Leopards ).

Washambulizi Michael Olunga (Al Duhail, Qatar), Masoud Juma (Difaa El Jadidi, Morocco), Moses Shummah (Kakamega Homeboyz), Benson Omalla (Gor Mahia).