logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wachezaji wa timu ya Argentina wajiunga na Lautaro Martinez katika harusi yake

Lautaro Martinez  alifunga ndoa Jumatatu na mpenzi wake wa muda mrefu  Agustina Gandolfo.

image
na

Makala30 May 2023 - 04:52

Muhtasari


• Mshindi huyo wa kombe la dunia akiwa na timu ya Argentina  tayari ana mtoto wa kike na mpenzi wake na anatarajia mtoto wa pili hivi karibuni.

• Licha ya mastaa wengi walio shinda naye kombe la Dunia kujitokeza na kujiunga naye katikA siku hii kubwa ukosefu wa  Lionel Messi aliubua gumzo kubwa mitandaoni.

Mchezaji wa Inter Milan na mchumba wake Agustina.

Mshambulizi  wa Inter Milan Lautaro Martinez  alifunga ndoa Jumatatu na mpenzi wake wa muda mrefu  Agustina Gandolfo.

Lautaro Martinez aliendelea kushinda nje ya uwanja siku nne tu baada ya kuisaidia timu yake ya Inter Milan kuibuka mabingwa wa Kombe la Italian na kuwafikisha katika fainali ya Klabu bingwa barani Ulaya.

Mshindi huyo wa kombe la dunia akiwa na timu ya Argentina  tayari ana mtoto wa kike na mpenzi wake na anatarajia mtoto wa pili.

 Kama ilivyoripotiwa na Gazzetta.it, wapenzi hao walifunga ndoa huko Villa d'Este kwenye Ziwa Como mbele ya wageni 120.

Miongoni mwa wageni tajika katika harusi yake ni wachezaji wenzake katika timu ya taifa ya Argentina wakiwemo Enzo Fernandez, Alexis Emiliano Martinez, Nicholas Tagliafico na kiungo wa Brighton Alexis MacAllister.

Pia mshambulizi mwenzake katika klabu ya Inter Millan Romelu Lukaku walijiunga naye akiwa ameandamana na mwanamuziki Meghan The Stallion na kuibua mjadala kuwa wawili hao walikua kwenye mahusiano.

Miongoni mwa wachezaji wa timu ya Nerazzurri waliokuwepo ni Roberto, Tucu Correa, Edin Dzeko, Stefan De Vrij, Danilo D'Ambrosio, Samir Handanovic na makamu wa rais Javier Zanetti.

 Pia kulikuwa na mchezaji mkubwa wa zamani wa Nerazzurri, Achraf Hakimi, ambaye alibaki karibu sana na timu hiyo ya Milan licha ya kuhamia  PSG.

Licha ya mastaa wengi walio shinda naye kombe la Dunia kujitokeza na kujiunga naye katika siku hii kubwa ukosefu wa  Lionel Messi aliibua gumzo kubwa mitandaoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved