Dabo kuondoka Coventry baada ya kukosa penalti katika fainali

Fankaty Dabo kuondok Conventry siku chache baada ya kukosa penalti katika mchuano wa fainali ya mchujo wa kupanda daraja

Muhtasari

• Coventry katika taarifa kwenye tuvuti yake ilithibitisha kuwa Fankaty Dabo ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu.

• Luton ilipanda hadi Ligi kuu ya Uingereza baada ya kushinda 6-5 kwenye mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 baada ya dakika 120.

Mchezaji wa Conventry City Dabo Fankaty baada ya kupoteza penalti
Mchezaji wa Conventry City Dabo Fankaty baada ya kupoteza penalti
Image: HISANI

Fankaty Dabo ameondoka Converty City baada ya kupoteza penalti katika fainali ya mchujo wa kupanda daraja ya ligi kuu nchini uingereza.

Coventry katika taarifa kwenye tuvuti yake ilithibitisha kuwa Fankaty Dabo ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu siku chache baada ya kukosa penalti katika mchuano wa fainali ya mchujo wa kupanda daraja dhidi ya Luton katika Uwanja wa Wembley Jumamosi.

Luton ilipanda hadi Ligi kuu ya Uingereza baada ya kushinda 6-5 kwenye mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 baada ya dakika 120. 

Dabo, ambaye amekuwa na klabu hiyo tangu 2019, anaungana na Julien Dacosta, Todd Kane, Sean Maguire, Michael Rose, Martyn Waghorn na Tyler Walker kuondoka klabu hio ya Conventry city mikataba yao itakapomalizika. 

Meneja wa Coventry Mark Robins aliwashukuru walioondoka, na akatoa pongezi kwa Dabo na Rose kwa majukumu yao muhimu katika ushindi wa taji la Ligi ya daraja ya Kwanza ya 2019/20. 

"Ningependa kuwashukuru wale ambao wanaondoka, michango kwa klabu Coventry City, na ninawatakia kila la heri kwa maisha yao ya baadaye," Robins alisema katika tovuti ya Coventry Jumanne. 

"Hasa, Fankaty Dabo na Michael Rose walikuwa sehemu kubwa ya timu ambayo ilishinda taji la Ligi ya Kwanza na kutupandisha ngazi hadi ligi ya championship.