logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu maana ya mpira na jezi maalum FIFA walimpa Straika wa Napoli Victor Osimhen

"Victor Osimhen, unawakilisha kwa sasa kile ambacho mpira wa miguu unaweza kufanya," - FIFA.

image
na Davis Ojiambo

Michezo08 June 2023 - 14:14

Muhtasari


  • • Osimhen alikuwa muhimu kwa Napoli kushinda taji la Serie A maarufu Scudetto kwa mara ya kwanza baada ya miaka 33.
  • • Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao 26 na kusajili asisti nne katika mechi 32 za ligi akiwa na Partenopei.
FIFA wampa Osimhen jezi maalum na moira, maana yake ni ipi?

Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA, limemzawadia mshambuliaji wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen jezi maalum na mpira kufuatia uchezaji bora wa mshambuliaji huyo katika klabu ya Napoli msimu wa 2022/23.

Osimhen alikuwa muhimu kwa Napoli kushinda taji la Serie A maarufu Scudetto kwa mara ya kwanza baada ya miaka 33.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao 26 na kusajili asisti nne katika mechi 32 za ligi akiwa na Partenopei.

Mshambulizi huyo pia alitikisa nyavu mara tano katika mechi sita alizoichezea klabu yake katika michuano ya UEFA Champions League.

Osimhen alishinda tuzo ya mfungaji bora wa Serie A, Mwafrika wa kwanza kufikia mafanikio hayo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Wolfsburg pia alitajwa kuwa mshambuliaji bora na kujumuishwa kwenye Timu bora ya Msimu.

"Victor Osimhen, unawakilisha kwa sasa kile ambacho mpira wa miguu unaweza kufanya," FIFA iliandika katika ujumbe kwa mchezaji huyo.

"Kutoka Lagos hadi Napoli ambako watu wanakupenda, umeteseka, lakini upendo wako kwa soka na uamuzi umekuongoza. Endelea, endelea kusukuma. Afrika inahitaji mifano na mamilioni wanakutazama na kuota kuwa kama wewe.”

Osimhen alianza uchezaji wake wa kulipwa rasmi nchini Ujerumani mnamo 2017 na VfL Wolfsburg. Baada ya kukaa kwa msimu mmoja na nusu na timu hiyo, alihamia kwa mkopo Charleroi ya Ubelgiji mnamo 2018-19 kabla ya kujiunga na Lille ya Ufaransa.

Akiwa na klabu hiyo ya Ufaransa, alicheza mchezo wake wa kwanza wa soka la Uropa katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA 2019-20. Osimhen alihamia timu ya Serie A Napoli mnamo 2020 kwa rekodi ya kilabu ya Euro milioni 70.

Katika msimu wa 2021-22, alitajwa kuwa Mchezaji Bora Chipukizi katika Serie A. Sasa anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi na Mwafrika katika msimu mmoja na ndiye mfungaji bora zaidi kati ya Waafrika kwenye Serie A.

 

Mnamo 2015, Osimhen alipewa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu cha Kombe la Dunia la FIFA U-17, ambayo Nigeria ilishinda. Alishiriki Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 na akacheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mnamo Juni 2017. Kwa sasa anashika nafasi ya nane kwa muda wote kati ya wafungaji mabao wa timu ya taifa ya Nigeria.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved