logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Migori Youth yalalamikia madai Kupanga matokeo ya mechi katika ligi ya NSL

Timu ya Migori Youth FC imelalamikia kupanga kwa matokeo ya mechi katika ligi NSL.

image
na

Makala13 June 2023 - 06:03

Muhtasari


• Klabu hiyo ilisema kuwa imepatwa na mshangao baada ya matukio katika ligi hiyo ya National Super League katika mechi za Jumapili na Jumatatu.

• Katika malalamisha hayo,timu hiyo inayoshikilia nambari ya nne ilitilia shaka hatua ya klabu ya Kibera Black Stars kutocheza mechi iliyopangwa kuchezwa jumapili katika uwanja wa Migori.

Wachezaji wa Migori Youth FC.

Timu ya ligi ya daraja ya pili National Super League (NSL), Migori Youth FC imelalamikia kupanga kwa matokeo ya mechi katika ligi hiyo.

Katika taarifa waliyochapisha kwenye ukurasa wao Facebook, Migori Youth FC waliibua tetesi za kupanga matokeo ya mechi dhidi ya Klabu za Kibera Black Stars na Silibwet.

Klabu hiyo ilisema kuwa imepatwa na mshangao baada ya matukio katika ligi hiyo ya National Super League katika mechi za Jumapili na Jumatatu.

“Usimamizi wa Timu ya Migori Youth FC imetazama kwa mshtuko matukio katika ligi ya National Super League haswa katika raundi za mechi zilizochezwa ama kupangwa kuchezwa kati ya Jumapili tarehe 11 Juni na Jumatatu tarehe 12 mezi Juni,” ilisoma sehemu ya taarifa hiyo.

Katika malalamisha hayo,timu hiyo inayoshikilia nambari ya nne ilitilia shaka hatua ya klabu ya Kibera Black Stars kutocheza mechi iliyopangwa kuchezwa jumapili katika uwanja wa Migori.

Kulingana na wawikilishi hao wa kaunti ya Migori, klabu ya Kibera Black Stars haijawai susia kucheza mechi yoyote iliyopangwa tangu wajiunge na ligi hiyo msimu wa 2017/2018.

Timu ya Migori Youth waliweza kupewa pointi tatu na mabao mawili baada ya mechi hiyo kukosa kuchezwa.

Madai hayo pia yalielekezwa kwa timu ya Silibwet ambao katika taarifa hiyo walidaiwa kukubali kichapo cha mabao saba dhidi ya Mara Sugar FC amabao walihitaji mabao saba ili kuwapiku wenzao Migori Youth FC na kuwapeleka hadi nafasi ya tatu.

Timu hiyo ya Silibwet ilikumbwa na madai ya kupanga matokeo katika mechi mbili za msimu huu katika mechi yao dhidi ya Kibera Black Stars na Shabana. Ndani ya mechi hizo mbili timu hiyo ilifungwa mabao sita kwa njia yakutiliwa shaka.

Timu hiyo yenye matumaini ya kupandishwa daraja kuelekea ligi kuu ya taifa KPL, ilisema uamuzi wa shirikisho la soka nchini FKF kuwa hakuna timu itakayoshushwa daraja katika ligi hiyo ya NSL uliathiri matokeo katika mechi dhidi ya timu zilizoshikilia mkia na timu zilizokuwa zikipigania kupandishwa daraja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved