Lionel Messi akamatwa na polisi nchini Uchina

Messi alifika China kucheza mechi iliyoratibiwa dhidi ya Australia kwenye Uwanja wa Workers Stadium mnamo Juni 15.

Muhtasari

• Kwa mujibu wa baadhi ya taarifa, mara tu Messi alipofika China kuiongoza Argentina katika mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu dhidi ya Australia, alijikuta akiingia matatani na Polisi wa Mpaka wa China.

Lionel Messi akamatwa na polisi wa Uchina.
Lionel Messi akamatwa na polisi wa Uchina.
Image: Screengrabs

Jumanne kulikuweko na picha mitandaoni pamoja pia na habari zilizoenezwa kwamba mchezai namba moja wa soka kwa muda wote, raia wa Argentina Lionel Messi alitiwa mbaroni na maafisa wa uwanja wa ndege nchini Uchina.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo hazikuwa zimedhibitishwa, mchezaji huyo alitiwa nguvuni kuhusiana na masuala yaliyoambatanishwa na Visa ya kusafiria.

Taarifa hizo pia zilidai kwamba mtafaruku huo ulidumu kwa takribani dakika 30, huku Messi akiwa chini ya ulinzi mkali jijini Beijing.

Messi alifika China kucheza mechi iliyoratibiwa dhidi ya Australia kwenye Uwanja wa Workers Stadium mnamo Juni 15.

Kwa mujibu wa baadhi ya taarifa, mara tu Messi alipofika China kuiongoza Argentina katika mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu dhidi ya Australia, alijikuta akiingia matatani na Polisi wa Mpaka wa China.

Suala lililoripotiwa lilihusu visa yake, kwani Messi alikuwa akishikilia pasipoti ya Uhispania badala ya pasipoti yake ya Argentina bila visa halali ya Uchina.

“Suala hilo lilidumu kwa takriban dakika 30 na baadaye kutatuliwa na kumruhusu Messi kuendelea na safari yake nje ya uwanja wa ndege,” chanzo kimoja cha habari kilisema.

Argentina inatazamia kupanda kinyang'anyiro cha kuwania kombe la dunia dhidi ya Australia mnamo Juni 15. Baada ya hapo wataondoka kuelekea Indonesia, ambako watacheza dhidi yao Juni 19.

Messi, ambaye anashikilia mataji yote makubwa ya soka, aliwashangaza mashabiki wake mwezi uliopita kwa kuondoka Paris Saint Germain (PSG) mwishoni mwa kandarasi yake na kujiunga na Inter Miami.

Nyota huyo wa Argentina aliamua kuacha soka la Ulaya na kuchezea Inter Miami baada ya miezi michache tu baada ya kushinda Kombe la Dunia la FIFA 2023 nchini Qatar.

Messi kwa sasa yuko mapumzikoni kabla ya kuanza sura mpya ya maisha yake. Messi anatazamiwa kujiunga na Inter Miami, timu ya Ligi Kuu ya Soka (MLS) inayomilikiwa na David Beckham, katika jiji la Miami.

Alijiunga na PSG mnamo 2021 baada ya kumaliza miaka yake ishirini na Barcelona. Sasa ameamua kutoongeza mkataba na PSG na ataachana na soka la Ulaya kwenda kucheza na Inter Miami.