Sweden: Wachezaji wa kike walilazimishwa kuonyesha nyeti zao kudhibitisha jinsia zao

"Wakati kila mtu kwenye timu yetu alichunguzwa, ambayo ni kusema, amefunua uke wake, daktari wa timu yetu alisaini kuwa timu yetu inajumuisha wanawake pekee."

Muhtasari

• Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa kombe la dunia ambapo wachezaji wa kike wa Uswidi wote walitakiwa kuvua nguo zao ili kuonesha nyeti zao kudhibitisha kuwa wao ni wanawake.

Timu ya taifa la wanawake Uswidi ililazimishwa kuonesha uke wao kushibitisha kuwa wao ni wa jinsia ya kike, mchezaji mmoja amedhibitisha kupitia mswada wa kitabu chake.
Timu ya taifa la wanawake Uswidi ililazimishwa kuonesha uke wao kushibitisha kuwa wao ni wa jinsia ya kike, mchezaji mmoja amedhibitisha kupitia mswada wa kitabu chake.
Image: Screengrab

Mchezaji kandanda wa kike kutoka Sweden Nilla Fischer amefichua kuwa timu ya taifa ya wanawake ililazimishwa kuvua nguo na 'kuonyesha sehemu zao za siri' kwa madaktari ili kuthibitisha kuwa walikuwa wa kike kwenye Kombe la Dunia la Wanawake 2011 nchini Ujerumani.

'Tuliambiwa kwamba hatupaswi kunyoa ''chini'' katika siku zijazo na kwamba tutaonyesha sehemu zetu za siri kwa daktari,' Fischer aliandika katika kitabu chake kipya cha 'I Didn't Even Say Half Of It', kulingana na jarida la Mail.

'Hakuna anayeelewa jambo kuhusu kunyoa lakini tunafanya kama tunavyoambiwa na kufikiri ''imefikiaje hili?'' Kwa nini tunalazimika kufanya hivi sasa, lazima kuwe na njia nyingine za kufanya hivi. Je, tunapaswa kukataa?

"Wakati huo huo hakuna anayetaka kuhatarisha fursa ya kucheza Kombe la Dunia. Ni lazima tu tufanye uchafu hata kama unahisi kuumwa na kufedheheshwa.'

Beki huyo wa kati wa Uswidi ambaye aliichezea nchi yake mechi 194, alifunguka zaidi kuhusu uzoefu huo katika mahojiano na gazeti la Aftonbladet la Uswidi.

"Ninaelewa ninachopaswa kufanya na kushusha haraka suruali yangu ya mazoezi na chupi kwa wakati mmoja," alisema.

'Mwanafizio anaitikia kwa kichwa na kusema ''yup'' kisha anamtazama daktari ambaye amesimama na mgongo wake kwenye mlango wangu. Anaandika na kusogea kwenye korido ili kugonga mlango unaofuata.

"Wakati kila mtu kwenye timu yetu anachunguzwa, ambayo ni kusema, amefunua uke wake, daktari wa timu yetu anaweza kusaini kuwa timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Uswidi inajumuisha wanawake pekee."

Wiki mbili kabla ya michuano hiyo kuanza nchini Ujerumani, FIFA ilitoa sera zake mpya za utambuzi wa kijinsia ambazo zimesalia kutumika leo.

Sheria zinataka timu zitie saini tamko linalosema kwamba wachezaji wote wanaoshiriki mashindano hayo ni 'wa jinsia inayofaa'.

Ukaguzi ulitekelezwa wakati timu za Nigeria, Ghana na Afrika Kusini zilipopinga kutokana na uvumi kwamba baadhi ya wachezaji waliochezeshwa na Equatorial Guinea wanaweza kuwa wanaume.

Lakini haijulikani kwa nini wachezaji walilazimishwa kuonyesha sehemu zao za siri, badala ya kuwasilisha mtihani rahisi wa swab kwa uchunguzi kama ilivyo kawaida.

Fischer alisema kuwa uchunguzi huo uliofanywa na wataalamu wa timu kunamaanisha wachezaji hao walipitia majaribu hayo katika ‘mazingira salama’, lakini ni wazi kuwa hakufurahishwa na jinsi hali hiyo ilivyoshughulikiwa.

"Tulikuwa na mazingira salama sana katika timu. Kwa hivyo pengine yalikuwa mazingira bora zaidi ya kuifanya. Lakini ni hali ya ajabu sana na kwa ujumla si njia nzuri ya kuifanya.”

FIFA ilisema 'imezingatia maoni ya hivi majuzi yaliyotolewa na Nilla Fischer kuhusu uzoefu wake na upimaji wa uhakiki wa jinsia uliofanywa na timu ya taifa ya Uswidi kwenye Kombe la Dunia la Wanawake la 2011' kujibu mahojiano ya Fischer.