Mshambuliaji wa Brazili, Neymar Jr amefichua sababu zinazomfanya kuhisi kwamba bara la Afrika litahitaji miaka mingi Zaidi ili kushinda taji lao la kwanza katika masindano ya kombe la dunia, ikiwa ni Zaidi ya miaka 90 tangu kuzinduliwa kwa mashindano hayo makubwa Zaidi ya soka.
Kulingana na mwanasoka huyo, Afrika haiwezi shinda kombe la dunia hadi pale wachezaji wake watakapokubali kuweka mapenzi yao nyuma ya jezi za mataifa yao.
Neymar anahisi kwamba wachezaji wengi hawapendi kuwajibikia mataifa yao na ndio maana mataifa yao yanaishia kuboronga katika mashindano ya kimataifa kwan iwachezaji wao wengi hujipata wakiwakilisha mataifa ya kigeni ambayo si yao ya kuzaliwa.
Neymar alikiri kwamba bara la Afrika kwa miongo kadhaa limekuwa likitoa wachezaji wenye hadhi za juu lakini wachezaji hao huishia kuchezea mataifa ya nje ya Afrika.
“Afrika haishindi kombe la dunia kwa sababu wachezaji wa Kiafrika huchezea mataifa ya Ulaya. Hili ni tofauti na sisi Brazili kwa sababu sisi haijalishi kwenye tunafanyia mazoezi, ni sharti tuweke mapenzi na kuipambania jezi ya Brazili kivyovyote vile,” alisema.
“Wachezaji wa Kiafrika wana talanta, lakini hawaioneshi kwa timu za mataifa yao. Wachezaji wa Kiafrika hawana ule msukumo Zaidi wa kuyawakilisha mataifa yao kama inavyokuwa kwa wachezaji wa mataifa ya Amerika Kusini, na ndio maana Brazili tuna mataji 5 ya kombe la dunia,” Neymar aliambia FirstMag LeVrai.
Licha ya mashindano hayo kuzinduliwa mapema miaka ya 1990s, kihistoria hakuna taifa la bara Afrika ambalo limewahi shinda taji hilo, taifa lililofanya bora Zaidi likiwa ni Morocco kufika nusu fainali katika kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar.