logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Senegal yalaza Brazil katika mechi ya kirafiki

Timu ya Senegal ilitoka nyuma na kulaza Brazil 4-2 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.

image
na Davis Ojiambo

Michezo21 June 2023 - 07:08

Muhtasari


  • • Mabingwa hao wa Afrika waliwagaragaza Brazil, baada ya Sadio Mane kufunga mabao mawili, Brazil ilikuwa ya kwanza kufunga bao katika dakika kumi ya kwanza.
  • • Lucas Paqueta aliwafungia Brazil kwa kichwa akiunganisha krosi ya Vinicius Junior ndani ya dakika 10 za kwanza, lakini Senegal walisawazisha kupitia mkwaju wa Habib Diallo.
Wachezaji wa Senegal wakisherekea ushindi wao dhidi ya Brazil Jumanne.

Timu ya taifa ya Senegal ilitoka nyuma na kulaza Brazil 4-2 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa mjini Lisbon Jumanne.

Mabingwa hao wa Afrika waliwagaragaza miamba hao wa soka duniani baada ya Sadio Mane kufunga mabao mawili, Brazil ilikuwa ya kwaonza kufunga bao katika dakika kumi za kwanza.

Mabingwa hao mara tano wa Kombe la dunia bado hawana kocha baada ya kuondoka kwa Tite mwaka jana baada ya kubanduliwa katika robo fainali ya kombe la dunia la mwaka 2022.

Brazil walikosa huduma za mshambulizi wao matata  Neymar huku mshambulizi huyo akisalia nje ya uwanja kutokana na jeraha la kifundo cha mguu alilopata mwezi Februari.

Lucas Paqueta alifungia Brazil kupitia mkwaju wa kichwa akiunganisha krosi ya Vinicius Junior ndani ya dakika 10 za kwanza, lakini Senegal walisawazisha kupitia mkwaju wa mshambulizi wa Strasbourg, Habib Diallo.

Marquinhos aliweka Senegal mbele mapema katika kipindi cha pili wakati beki huyo wa Paris Saint-Germain alipojifunga.

Mane, ambaye alikosa Kombe la Dunia kutokana na jeraha na kuwa na msimu mgumu akiwa Bayern Munich, aliongeza bao lingine dakika ya tatu baadaye.

Brazil walipunguza tofauti ya mabao wakati Marquinhos wakati huu alipofunga bao na kumpita kipa wa Senegal, Mory Diaw.

Lakini Mane alihakikishia Senegal ushindi katika dakika za lala salama alipofunga bao lake la pili kwenye mchezo huo kwa mkwaju wa penalti.

Ushindi huu wa unamaanisha kuwa Brazil hawajaandikisha ushindi wowote dhidi ya Senegal baada ya mechi zao mbili zilizopita. Mechi ya kwanza baina ya timu hizi mbili iliisha sare.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved