SOKA YA FKF

Meneja msaidizi wa Kakamega Homeboyz adokolewa meno matatu

Waliomvamia walihisi kuwa alisaidia Kakamega Homeboyz kuishinda Gor

Muhtasari

• Kabumbu ni mchezo ambao unafurahisha watu, na mnakuwa tu wapinzani kwa dakika tisini, mpira ukiisha, mnakubali aliyeshinda anafurahia na wakushindwa ajue kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.

Meneja msaidizi wa Kakamega Homeboyz baada ya kuvamiwa ugani Moi
Meneja msaidizi wa Kakamega Homeboyz baada ya kuvamiwa ugani Moi
Image: Peter Atwenge//Twitter

 Juni 21, katika uwanja wa michezo wa Moi, palitokea kivumbi baada ya mechi kati ya Kakamega Homeboyz na Gor Mahia, ambapo vurugu ilizuka na kusababisha kuvamiwa kwa Meneja Msaidizi wa timu ya Kakamega Homeboyz aliyeng’olewa meno matatu.

Kulingana na tukio hilo, kumeibuka tetezi kuwa waliomvamia walihisi kwamba alisaidia timu yake kuishinda Gor ambapo walipoteza mechi hiyo licha ya kuongoza kipindi cha kwanza kwa mabao mawili kwa bila.

Peter Atwenge, baada ya uvamizi huo alielekea katika kituo cha polisi kuripoti tukio hilo ambalo pia limekashifiwa vikali na baadhi ya mashabiki. Haijabainika ni kina nani waliomshambulia, ila jawabu litachipuka baada ya polisi kuanzisha na kukamilisha uchunguzi wao.

Kulingana na maoni ya aliyekuwa mkufunzi wa Harambee Stars Jacob Mulee, amelikosoa sana tendo hilo na ambapo amekiri kuwa , hajafurishwa na vurugu hiyo akidai asiyekubali kushindwa si mshindani watu wanapaswa kufurahia kabumbu na pia wakubali matokeo.

“Tumekuwa tukiona vurugu katika mpira na mimi sijafurahia sana kuona vurugu baada ya mechi, labda mtu kuumzwa, mpira unafaa kuleta watu pamoja,  kabumbu ni mchezo ambao unafurahisha watu na mnakuwa tu wapinzani kwa dakika tisini, mpira ukiisha, mnakubali aliyeshinda anafurahia na wakushindwa ajue kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.” Mulee alisema.

Haya yanajiri wakati ambapo Gor Mahia walihitaji kuzinyakuwa alama tatu katika mechi hiyo ili kuuthibi ubingwa wao katika ligi ya FKF na iwapo wapinzani wao Wanamvinyo Tusker FC wangepoteza.

Kupoteza kwa Gor katika mechi hiyo ina maana watalazimika kupata ushinda katika mechi inayofuata, na kisha kuwaombea njaa wapinzani wao.