logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamie Carragher ataka Saudi ichunguzwe juu ya uhamisho

Walimchukua Ronaldo, Benzema, Kante, na sasa wananyapia kumnyakua Bernado Silva miongoni mwa wengine.

image
na

Yanayojiri23 June 2023 - 05:14

Muhtasari


• “ Sikuogopa wakati ligi ya Saudi walipokuwa wakichukua wachezaji waliokuwa katika miaka yao ya 30, ila, naogopa kwa wachezaji waliochini, (Neves)  lakini hili likifanyika, itahisiwa kama “Game Changer.”

Mchanganuzi wa masuala ya soka nchini Uingereza Jamie Carragher ametoa wito kwa ligi ya Premier na UEFA kuchunguza Saudi Arabia, kuhusiana na uhamisho wa wachezaji unaoendelea katika taifa hilo msimu huu wa joto.

Haya yanajiri kutokana na tetesi za hivi punde, katika taifa hilo za kiungo wa mabingwa Uingereza Manchester City, Bernado Silva kuhusishwa na kukamilisha kujiunga katika ligi hiyo inayojulikana kama Saudi Pro League.

Katika mtandao wake wa Twitter Carragher aliposti, “ Bernado Silva yupo katika miaka yake ya juu zaidi na amekuwa mchezaji bora zaidi katika Uropa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Sikuogopa wakati ligi ya Saudi walipokuwa wakichukua wachezaji waliokuwa katika miaka yao ya 30, ila, naogopa kwa wachezaji waliochini, (Neves)  lakini hili likifanyika, itaonekana kama “Game Changer”.

Saudi wamechukua Golf, Mashindano makubwa ya Boxing na sasa wanataka kuchukua kandanda. Utapeli huu katika mchezo unahitaji kukomeshwa.

Tangu Cristiano Ronaldo kujiunga na ligi hiyo, baadhi ya wachezaji bara Uropa wamekuwa wakitamani kujiunga na Saudi, hasa ikifahamika ofa inayotolewa katika malipo yao ni bora kuliko ya Uingereza.

Saudi, tayari wamemchukua aliyekuwa mshambulizi wa Real Madrid Karim Benzema, N’golo Kante wa Chelsea na sasa wananyapia kumnyakua Bernado Silva wa Man City, miongoni mwa wengine wanaohusishwa kujiunga na ligi hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved