SOKA KIMATAIFA

Kyle Walker aorodheshwa miongoni mwa wachezaji wenye kasi zaidi Uingereza

Beki huyo pia aliweka rekodi ya kutofungwa kama mlindalango 2019 katika mechi moja

Muhtasari

• Baadhi ya wanasoka wengine ambao ni wapinzani wake wa karibu kwenye kasi ni pamoja na; Brennan Johnson wa Nottingham Forest 36.7km/h, Mykhailo Mudryk wa Chelsea 36.63km/h, Anthony Gordon wa Everton 36.6km/h miongoni mwa wengine.

Image: Kyle Walker//Twitter

Beki wa Manchester City Kyle Walker ameorodheshwa kuwa wa kwanza miongoni mwa wachezaji walio na mbio sana katika ligi kuu Uingereza.

Walker, 33, katika msimu uliotamatika wa 2022/2023 aliweka rekodi ya 37.31 km/h, akikwea jukwaani mwa rekodi zingine zilizorekodiwa.

Baadhi ya wanasoka wengine ambao ni wapinzani wake wa karibu kwenye kasi ni pamoja na; Brennan Johnson wa Nottingham Forest 36.7km/h, Mykhailo Mudryk wa Chelsea 36.63km/h, Anthony Gordon wa Everton 36.6km/h miongoni mwa wengine.

Licha ya umri wake wa zaidi ya miaka 30, Walker amekuwa mchezaji wa kufana zaidi chini ya ukufunzi wa meneja Guradiola, ambapo huwajibika kwa kiasi kikubwa anapotumiwa kama beki wa kulia.

Kyle Walker amesaidia klabu hiyo wakati beki mshambulizi Nathan Ake alipopata jeraha katika michuano ya ligi ya mabingwa, alipomthibiti Vinicius Jr, pamoja na mawinga wengine wanaodhaniwa kusambaratisha mabeki, hasa mabeki wa kulia.

Kama miongoni mwa wachezaji wa wabingwa wa “Treble” tangu ajiunge na Man City kutoka klabu la Tottenham Hotspurs 2017, Mwingereza huyo ameshinda mataji 12 kwa jumla ikilinganishwa na miaka ya awali alipochezea Aston Villa na Spurs bila kunyakua taji lolote.

Kando na hayo, Walker aliweka kumbukumbu za kihistoria katika klabu ya Man City, alipotumika kama mlindalango katika mechi yao ya ligi ya mabingwa dhidi ya Atalanta mwaka wa 2019.

Kulingana na Pep Guardiola, alimtumia Walker baada ya Claudio Bravo kutumwa nje kwa kadi nyekundu, naye Ederson chaguo la kwanza langoni enzi hizo alikuwa amekumwa na jeraha.

Katika kumbukumbu, Walker alicheza katika dakika zilizokuwa zimesalia, ambapo aliweka “clean sheet” hadi mechi hiyo ilipotamatika.