Mourinho ajitolea kuifufua nyota ya Greenwood katika soka ambapo kila mtu hamtaki

Itakumbukwa Greenwood yuko na mkataba na United hadi mwaka 2025, lakini kama ambavyo mambo yamesimama itakuwa vigumu sana kwake kuweza tena kuichezea timu hiyo ya Old Trafford.

Muhtasari

• Mnamo 2018, Mourinho alimchagua Greenwood kama kijana wa miaka 16 kwenda kwenye ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya huko Merika.

• Mourinho aliwasiliana na nyota huyo matata wa Manchester United kuhusu kujiunga na klabu hiyo ya Serie A kwa mkopo.

Mourinho kumchukua Greenwood Roma
Mourinho kumchukua Greenwood Roma
Image: Twitter

Mason Greenwood amepewa ofa ya maisha ya soka - na bosi wake wa zamani Jose Mourinho huko Roma, jarida la The Sun limeripoti.

Mourinho aliwasiliana na nyota huyo matata wa Manchester United kuhusu kujiunga na klabu hiyo ya Serie A kwa mkopo.

Greenwood bado amesimamishwa kazi huku wakuu wa United wakichunguza mwenendo wake kufuatia kukamatwa kwake Januari 2022 ili "kuamua hatua zinazofuata".

 

Greenwood, 21, alishtakiwa kwa jaribio la ubakaji, kujihusisha na tabia ya kudhibiti na kulazimisha na kushambulia.

 

Lakini polisi walithibitisha mnamo Februari kwamba Greenwood "hakabiliwi tena na kesi ya jinai" kwani Huduma ya Mashtaka ya Crown ilikuwa imefuta mashtaka yote.

 

Fowadi huyo wa Uingereza anaamini kuwa haiwezekani kuanza tena United, licha ya meneja Erik ten Hag na wachezaji wenzake kadhaa kumpa usaidizi.

Lakini Mourinho ana uhusiano mkubwa na Greenwood baada ya kumpa nafasi kama kocha wa Red Devils.

Mnamo 2018, Mourinho alimchagua Greenwood kama kijana wa miaka 16 kwenda kwenye ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya huko Merika.

Mapema wiki jana tuliripoti kwamba Greenwood aliondolewa kwenye tovuti rasmi ya timu ya Manchester United na mashabiki hawawezi tena kuweka ombi la kuinunua jezi yake baada ya timu hiyo kuziondoa zote.

 Mustakabali wa Greenwood katika timu hiyo ya ujana wake unasalia katika hali ya ukungu na kiza kinene baada ya awali kuarifiwa kwamba watu kadhaa katika timu hiyo wamegawanyika kuhusu kurudishwa kwake timuni.

Mwaka jana, pia iliripotiwa kwamab timu ya wanawake ya Manchester United walipinga vikali Greenwood kurudishwa katika timu hiyo na hivyo kuweka maisha yake katika timu hiyo kuwa kwenye mstari mwekundu.

Iliarifiwa kwamba United walikuwa wanawazia kumtoa kwa mkopo nje ya Ulaya, katika kile walisema kuwa hakuna timu ambayo itamkubali kutokana na uzito wa madai yaliyokuwa yanamkabili kuhusu unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mpenzi wake.

Lakini licha ya taarifa hizo, Mourinho ambaye alimtambulisha katika timu rasmi ya United akimtoa kwenye academia amearifiwa kuguswa na hali yake na kujitolea kuififia tena ndoto na nyota yake kwa kumchukua kwa mkopo.

Itakumbukwa Greenwood yuko na mkataba na United hadi mwaka 2025, lakini kama ambavyo mambo yamesimama itakuwa vigumu sana kwake kuweza tena kuichezea timu hiyo ya Old Trafford.