Binti wa Eto'o ataka mchezaji huyo wa zamani kufungwa jela kwa kukataa kumpa matunzo

Binti huyio alizaliwa mwaka 1999 wakati Eto'o akiwa tineja wa miaka 18 tu akisakatia Espanyol. Inaarifiwa walikutana na mamake kwenye klabu na wakashiriki tendo mara moja tu na hawakuwahi onana tena.

Muhtasari

• Hata hivyo, hatimaye Eto'o alimtambua bintiye mnamo Februari 2022.

• Alitakiwa kumlipa malipo ya ziada ya kila mwezi, kwa kuwa hali yake ya kifedha si nzuri.

Bintiye ataka mchezaji wa zamani wa Camroon kufungwa.
Samwel Eto'o Bintiye ataka mchezaji wa zamani wa Camroon kufungwa.
Image: Facebook

Binti wa nguli wa Barcelona Samuel Eto’o anataka afungwe jela kwa kushindwa kulipa karo ya mtoto ya Euro 90,000., kiasi sawa na shilingi za Kenya Milioni 13.74, jarida la Sportskeeda limefichua.

Kulingana na gazeti la Uhispania la Sport, nguli wa Barcelona Samuel Eto'o anaweza kufungwa jela baada ya kushindwa kumlipa bintiye Erika de Rosario malipo ya kila mwezi ya Euro 1,400 kwa miaka mitano.

Erika, 22, alizaliwa na mpenzi wa zamani wa Eto'o Adileusa de Rosario. Gwiji huyo wa soka wa Cameroon, rais wa sasa wa shirikisho la soka nchini mwake, alichumbiana na Adileusa wakati akiwa mchezaji wa Real Madrid katika miaka ya 90.

Hata hivyo, hatimaye Eto'o alimtambua bintiye mnamo Februari 2022. Alitakiwa kumlipa malipo ya ziada ya kila mwezi, kwa kuwa hali yake ya kifedha si nzuri.

Wakati Eto'o anaishi maisha ya utele, hakumlipa binti yake pesa ya kumlea kwa miaka mitano, kumaanisha kwamba anadaiwa karibu €90,000. Wakili wa Erika, Fernando Osuna, alisema (kama ilivyo kwa El Diario de Sevilla):

"Anadaiwa zaidi ya miaka mitano ya pensheni kwa binti yake na anaendelea kukaidi haki. Uchumi wa Erika ni dhaifu, wakati Eto'o anaishi maisha ya anasa."

Osuna aliongeza:

"Anaweza kuhukumiwa kwa hali mbaya ya matumizi mabaya ya madaraka, kutokana na ubora wake kiuchumi kuliko Erika."

Kesi kuhusu kesi hiyo itafanyika mjini Madrid, Osuna alisema, huku mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Samuel Eto'o akijikuta kwenye maji ya moto.