Kylian Mbappé: 'Ni heshima' kuwa Cameroon

Nyota wa soka wa Ufaransa Kylian Mbappé anasema "anaheshimika" kuzuru Cameroon, nchi yake "ya asili".

Muhtasari

•"Nina furaha sana kuwa hapa," aliongeza, akisema kwamba watu wamemwonyesha "mapenzi" mengi.

•Nyota huyo wa kandanda alizingirwa na mamia ya mashabiki waliokuwa na shauku alipowasili Cameroon siku ya Alhamis

•Ni safari yake ya kwanza nchini Cameroon tangu akiwa kijana.

Kylian Mbappé alizaliwa huko Paris kwa baba wa Cameroon
Kylian Mbappé alizaliwa huko Paris kwa baba wa Cameroon
Image: BBC

Nyota wa soka wa Ufaransa Kylian Mbappé anasema "anaheshimika" kuzuru Cameroon, nchi yake "ya asili".

"Nina furaha sana kuwa hapa," aliongeza, akisema kwamba watu wamemwonyesha "mapenzi" mengi.

Hapo awali, mashabiki wa kandanda walielezea kwa BBC msisimko walionao kuhusu safari hiyo.

"Sote tumekuwa tukingojea wakati na hatimaye imefika," mtu mmoja aliambia kipindi cha redio cha BBC Newsday

"Ni msaada mkubwa kwa Cameroon, sio tu kwa Cameroon lakini kwa bara zima," shabiki huyo aliongeza. "Kuwa naye karibu kunaonyesha kuwa nyumbani ni nyumbani - lazima urudi nyumbani kwako."

Nahodha huyo wa kandanda wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 na mshambuliaji wa PSG - ambaye alizaliwa Paris, Ufaransa, kwa baba Mcameroon - pia alikutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Joseph Ngute siku ya Ijumaa, pamoja na maafisa wengine.

Ni safari yake ya kwanza nchini Cameroon tangu akiwa kijana.

Nyota huyo wa kandanda alizingirwa na mamia ya mashabiki waliokuwa na shauku alipowasili Cameroon siku ya Alhamis
Nyota huyo wa kandanda alizingirwa na mamia ya mashabiki waliokuwa na shauku alipowasili Cameroon siku ya Alhamis
Image: bbc

Nyota huyo wa kandanda alizingirwa na mamia ya mashabiki waliokuwa na shauku alipowasili Cameroon siku ya Alhamisi

Nyota huyo wa michezo pia amekuwa akikutana na wanamichezo wengine wa Cameroon, kama vile nyota wa MMA Francis Ngannou, ambaye alipigwa picha naye akitabasamu.

Pia alicheza mpira wa kikapu na nyota wa zamani wa Chicago Bulls, Joakim Noah kwenye uwanja wa Noah, ambapo alipigwa picha na umati wa watu waliokuwa wakifuatilia mchezo huo.

Baadaye alicheza soka dhidi ya timu ya Cameroon Vent d'Etoudi FC, Reuters inaripoti.

Mbappé pia anafanya kazi ya kibinadamu katika safari yake kwa niaba ya taasisi yake, ambayo inataka kuwasaidia vijana kufikia malengo yao.