Chelsea yazindua jezi mpya ya msimu 2023/2024

Jezi mpya iliyozinduliwa hata hivyo haikuwa na mfadhili wa mbele wa jezi baada ya mkataba na kampuni ya 3 kutamatika.

Muhtasari

• Wachezaji kama Reece James, Mykhailo Mudryk na Enzo Fernandez walishiriki katika uzinduzi wa jezi hizo pamoja na nyota wa zamani wa Chelsea Roberto Di Matteo na Dennis Wise.

• Ligi ya Premia pia imepiga marufuku kampuni za kamari kuwa wafadhili wa mbele kwenye jezi za msimu wa 2025-26.

Wachezaji wa sasa na wa zamani wa Chelsea wakiwa wamevalia jezi mpya ya msimu 2023/2024.
Wachezaji wa sasa na wa zamani wa Chelsea wakiwa wamevalia jezi mpya ya msimu 2023/2024.
Image: CHELSEA

Klabu ya ligi kuu ya Uingereza, Chelsea imezindua jezi mpya ya msimu 2023/2024 ambayo inafanana na jezi za karne ya 20.

Jezi mpya iliyozinduliwa hata hivyo haikuwa na mfadhili wa mbele wa jezi baada ya mkataba na kampuni ya 3 kutamatika.

Wachezaji kama Reece James, Mykhailo Mudryk na Enzo Fernandez walishiriki katika uzinduzi wa jezi hizo pamoja na nyota wa zamani wa Chelsea Roberto Di Matteo na Dennis Wise.

Mashabiki wa Chelsea wataweza kuzinunua jezi hizo kuanzia mwezi Agosti 16 katika maduka ya Chelsea ama kwenye mtandao wao.

Timu hiyo imepokea ofa kadhaa kutoka kwa kampuni ambazo zingependa kuifadhili, hata hvivyo ofa hizo hazijapolewa vyema na washikadau wa spoti nchini humo.

Mkataba wa kampuni ya filamu ya Paramount+ ulipingwa kwa madai kuwa hatua hiyo ingewakera wamiliki wa haki ya EPL.

Chelsea pia walikuwa karibu kuingia katika mkataba na kampuni ya kamari ya Stake, lakini hilo lilizua hisia kali kutoka kwa mashabiki na kuilazimu Chelsea kufutilia mbali dili hiyo.

Ligi ya Premia pia imepiga marufuku kampuni za kamari kuwa wafadhili wa mbele kwenye jezi za msimu wa 2025-26.

Uzinduzi huu wa Chelsea unakuja siku chache tu baada ya timu ya Manchester United, Liverpool, Newscastle, Brighton na Arsenali.

The Blues baada ya kumsajili Mauricio Pochettino kwa mkataba wa miaka miwili mwezi Mei watakuwa na matumaini ya kampeni bora zaidi baada ya matokea mabaya yaliyosajiliwa msimu wa 2022-23.

Pochettino tayari ameshaanza kazi yake na kutaka kikosi hicho kupunguzwa kabla ya msimu ujao, tayari Kai Havertz amejiunga na mahisumu wao wa London, Arsenal, wakati Mateo Kovacic amesajiliwa na Manchester City.