Messi aichoma PSG na kuonesha mapenzi ya dhati kwa Chelsea na ManCity Instagram

Rasmi Messi ameacha kuifuata PSG Instagram na kufuata timu nne pekee zikiwemo timu ya utotoni Barcelona, ​​Newell's Old Boys, Manchester City na Chelsea pekee.

Muhtasari

• Mchezaji huyo aliondoka kwa shari PSG baada ya miaka miwili na kutimukia zake Inter Miami na Marekani.

Image: INSTAGRAM// LIONEL MESSI

Mchezaji anayetajwa kuwa namba moja kwa soka kote ulimwenguni, Muargwentina Lionel Messi sasa ni rasmi ameacha kuifollow akaunti ya timu ya PSG kwenye Instagram ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kuondoka kwa njia ya kishari.

Hatua ya Messi kuacha kuifollow PSG kwenye Instagram imetajwa kuwa ni kutokana na jinsi ambavyo uongozi wa timu hiyo inayomilikuwa na mkwasi wa Uarabuni ilivyomfanyia katika siku zake za mwisho klabuni hapo mwezi Mei.

Ikumbukwe Messi alifungiwa kucheza mecho kadhaa za kumalizia msimu uliokamilika kama adhabu ya kile kilitajwa kuwa alikiuka taratibu za timu kwa kuenda katika ziara ya kujivinjari nchini Saudi Arabia licha ya kocha mkuu Christpher Galtier kuwa kinyume na ziara hiyo.

Messi alikataa kusaini mkataba mpya na vigogo hao wa Ligi ya Ufaransa na badala yake akaamua kujiunga na timu ya Inter Miami inayoshiriki ligi ya Marekani – Major League Soccer – timu inayomiliiwa na gwiji wa Manchester United David Beckham.

Utafutaji rahisi kwenye Instagram ya Messi unaonyesha kwamba anafuata vilabu vinne pekee kwenye jukwaa sasa - Barcelona, ​​Newell's Old Boys, Manchester City na Chelsea.

Leo hajawahi kucheza Uingereza lakini inaonekana timu pekee za Kiingereza ambazo angechezea ni zile anazofuata kwenye Instagram.

Inavyoonekana, Messi bado hajaifuata klabu yake mpya ya Inter Miami ambayo ufuasi wake kwenye Instagram umeongezeka tangu nyota huyo wa Barca asajiliwe.

Hivi karibuni Messi anatarajiwa kuzinduliwa rasmi kama mchezaji wa Inter Miami na timu hiyo iliripoti ongezeko kubwa la ufuasi Instagram pindi walipotangaza kumsaini Messi mwezi jana.

Wakati huo huo, PSG walikuwa waathirika wakubwa wa kuondoka kwa Messi, ambapo watu Zaidi ya milioni 3 waliokuwa wakiifuata kwenye Instagram kuacha kuifuata rasmi baada ya taarifa za Messi kuondoka.