Nani anafaa kuwa nahodha mpya wa Man Utd baada ya Maguire kupokonywa wadhifa huo?

Sasa Maguire amevuliwa unahodha na bila shaka ndiye beki wa kati chaguo la tano wa Erik ten Hag katika United.

Muhtasari
  • Wakati Manchester United ilipolipa rekodi ya £80m kumfanya Harry Maguire kuwa beki ghali zaidi duniani mwaka 2019, moja ya vivutio vikubwa ni uwezo wake wa kuongoza.
Harry Maguire
Image: KWA HISANI

Beki wa Uingereza Harry Maguire ameambiwa hatakuwa nahodha wa Manchester United msimu ujao - je huo ndio uamuzi sahihi? Na hilo linaacha wapi mustakabali wa Maguire Old Trafford?

Bruno Fernandes aliongoza kikosi hicho mara nyingi msimu uliopita - je, yeye ndiye mchezaji sahihi kuchukua adhfa huo? Au kuna mgombea mwingine ambaye Erik ten Hag anafaa kumchagua?

Wakati Manchester United ilipolipa rekodi ya £80m kumfanya Harry Maguire kuwa beki ghali zaidi duniani mwaka 2019, moja ya vivutio vikubwa ni uwezo wake wa kuongoza.

Ndani ya miezi mitatu baada ya kuwasili kutoka Leicester, Maguire alikuwa nahodha wa klabu hiyo ya Old Trafford kwa mara ya kwanza. Chini ya miezi mitatu baada ya hapo, Muingereza huyo alipewa kitambaa hicho kwa misingi ya kudumu baada ya Ashley Young kuhamia Inter Milan.

Sasa Maguire amevuliwa unahodha na bila shaka ndiye beki wa kati chaguo la tano wa Erik ten Hag katika United.

Huku Euro 2024 ikikaribia mwisho wa msimu huu ujao, kocha wa Uingereza Gareth Southgate amemwambia Maguire anahitaji kucheza mara nyingi zaidi ili kupata nafasi yake kwenye kikosi.

Vyanzo vya karibu na Maguire vimesisitiza kwa miezi kadhaa kuwa anataka kusalia United. Lakini kwa mwisho gani?

Vilabu vingine, ikiwemo West Ham, vinamtaka Maguire. Swali linapaswa kuulizwa, je, huu ni wakati wa kuondoka?