Benjamin Mendy asaini na klabu ya Lorient siku 4 baada ya kuondolewa mashtaka

Beki huyo aliondolewa mashtaka yote ya ubakaji dhidi yake ambapo mlalamishi aliambia mahakama kwamba Mendy aliwahi mwambia kuwa alishiriki mapenzi na wanawake 10,000.

Muhtasari

• Aliondolewa kwa kosa la kumbaka mwanamke na kujaribu kumbaka mwingine katika Mahakama ya Chester Crown siku ya Ijumaa.

Benjamin Mendy asaini kataba wa miaka 2
Benjamin Mendy asaini kataba wa miaka 2
Image: BBC NEWS

Beki wa zamani wa Man City Benjamin Mendy amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Ligue 1 ya Lorient.

Beki huyo wa kushoto alipatikana hana hatia ya ubakaji na jaribio la ubakaji katika Mahakama ya Chester Crown wiki iliyopita; mshindi mara tatu wa Ligi Kuu na bingwa wa Kombe la Dunia Mendy aliachiliwa na Man City mkataba wake ulipomalizika mwishoni mwa Juni; mkataba wa miaka miwili uliothibitishwa na klabu ya Ligue 1 siku ya Jumatano

Mapema mwaka huu mwanasoka huyo hakupatikana na hatia ya makosa ya ngono dhidi ya wanawake kadhaa lakini mahakama haikuweza kufikia uamuzi wa mashtaka hayo mawili na kesi hiyo ikasikilizwa tena.

Mendy, 29, alikua mlinzi ghali zaidi katika Premier League wakati City ilipolipa £52m kwa Monaco kwa ajili yake mwaka wa 2017.

Alishinda mataji matatu akiwa na City na alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 2018.

Mendy aliachiliwa na City mkataba wake ulipomalizika mwishoni mwa Juni, mara ya mwisho kuichezea klabu hiyo Agosti 2021.