Chelsea, Arsenal zawalazimishia wapinzani salamu za 'hi-5' kwenye mechi za pre-season

Timu zote mbili zilishuhudia sajili zao moya Kai Havertz kwa Arsenal na Christopher Nkuku kwa Chelsea wakitinga wavuni bao lao la kwanza kila mmoja kwenye uzi wa timu mpya.

Muhtasari

• Hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa kocha Mauricio Pouchettino kuiongoza Chelsea.

Cheslea na Arsenal wafana kweney pre-season.
PRE-SEASON Cheslea na Arsenal wafana kweney pre-season.
Image: FAACEBOOK

Timu za London, Chelsea na Arsenal zimeanza mechi za kujifua wakijiandaa kwa msimu mpya mwezi ujao.

Timu hizo usiku wa kuamkia Alhamisi kila moja ilikuwa inashiriki mechi yake ya kwanza katika kampeni ya pre-season nchini Marekani.

Kwa upande wao, Arsenal ambao walimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali la EPL msimu uliopita na amnao wametajwa kuimarisha kikosi chao kwa sajili ghali walikuwa wanacheza na  timu ya pamoja ya ligi ya Marekani MSL.

Chelsea, ambao walivurunda msimu uliopita na kumaliza nafasi ya kumi na mbili walikuwa katyika jimbo la Florida ambapo walikuwa wanacheza dhidi ya timu ya Wrexham.

Arsenal walipiga timu ya pamoja ya MSL kibano cha mabao 5 bila jibu huku straika wao matata Mbrazili Gabriel Jesus akifungua karamu ya mabao kunako dakika ya tano.

Leandro Trossard akiwapa wanabunduki bao la pili kunako dakika ya 23 kabla ya mapumziko na kiungo Muitaliano Jorginho alifunga mkwaju wa penalty dakika mbili tu katika kipindi cha pili.

Gabriel Martinelli alifunga bao la nne dakika ya 84 kabla ya sajili mpya kutokea Chelsea, Kai Havertz kumaliza udhia kwa bao la tano dakika za lala salama.

Kwa upande wao Chelsea, kocha mkuu Mauricio Pouchettinho alianza kazi rasmi kwa ushindi mnono ambao kikosi chake cha wachezaji wachanga kilimpa tabasamu.

Katika kikosi cha timu hiyo ambayo imeachia wengi wa wachezaji wake mahiri, wachezaji 9 wachanga walishiriki mechi yao ya kwanza na kinda Ian Maatsen alifunga mabao mawili kunako dakika ya 3 na 42 kabla ya kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele.

Kiungo wa academia Conor Gallagher alifunga bao la tatu kwa The Blues kunako dakika ya 80 naye sajili mpya Christopher Nkuku aliandikisha bao lake la kwanza kwenye uzi wa Chelsea kunako dakika 90 akitokea kwenye benchi.

Beki mahiri Ben Chilwell alimaliza udhia kwa kuzamisha bao la tano kunako dakika za mazidadi na kumpa Pouchettinho furaha katika mechi yake ya kwanza kama meneja wa miamba hao washindi mara mbili wa kombe la klabu bingwa barani ulaya.