Kipa wa zamani wa West Ham, Shaka Hislop aanguka na kuziria 'Live' kwa TV

Shaka Hislop alianguka hewani alipokuwa akichambua mechi kati ya Real Madrid na AC Milan huko California.

Muhtasari

• Mchambuzi huyo mwenye umri wa miaka 54 alikuwa akizungumza pamoja na mtangazaji mwenzake Dan Thomas alipojikwaa kinyumenyume kabla ya kuanguka kifudifudi uwanjani.

Mchezaji wa zamani wa WestHam, Shaka Hislop.
Mchezaji wa zamani wa WestHam, Shaka Hislop.

Kipa wa zamani wa West Ham, Shaka Hislop alianguka hewani alipokuwa akichambua mechi kati ya Real Madrid na AC Milan huko California.

Nyota huyowa ligi ya Premier alikuwa akifanya kazi kama mchambuzi wa kituo cha utangazaji cha Marekani cha ESPN alipoanza kuonekana mgonjwa.

Mchambuzi huyo mwenye umri wa miaka 54 alikuwa akizungumza pamoja na mtangazaji mwenzake Dan Thomas alipojikwaa kinyumenyume kabla ya kuanguka kifudifudi uwanjani.

Thomas aliomba usaidizi huku madaktari wakikimbia kumsaidia Hislop na kituo hicho cha runinga kikielekea katika mapumziko ya kibiashara.

ESPN baadaye ilituma ujumbe wa Twitter na kusema Shaka alikuwa "anajifahamu na anazungumza" na alikuwa akihudumiwa na madaktari.

Hali ya kijoto huko California iliripotiwa kuwa karibu  nyuzi joto 30 siku ya Jumapili.

Katika sasisho la muda wa mapumziko, Thomas alisema: "Ni wazi mwenzangu, Shaka, hayuko hapa, lakini kama ilivyo sasa, ni habari njema."

Tangazo "Ana fahamu, anaongea, nadhani ana aibu kidogo juu ya yote. Ameomba msamaha sana - sio mtu anayependa watu kumfanyia mzaha."

Hislop alihudumu kwa vipindi viwili tofauti akiwa West Ham kuanzia 1998-2002 na 2005-2006. Pia alichezea Newcastle na Trinidad na Tobago.