Aliyekuwa mchezaji wa Manchester City David Silva ametangaza kustaafu katika kandanda akiwa na miaka 37.
Silva aliutangaza uamuzi huo baada ya kupata jeraha la goti, ambalo madaktari wake walisema kuwa jeraha hilo huenda likachukua muda mrefu sana kabla ya kupona, ambapo walisema linaweza kuchukua hata msimu mmoja.
Inaaminika kuwa kiungo huyo mshambulizi alipata jeraha hiyo katika mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya kuanza msimu mpya na klabu ya Real Sociedad ambako ameitumia kwa misimu mitatu.
Katika mtandao wake wa Twitter, mwanasoka huyo aliposti ujumbe akiwaaga wenzake katika ulumwengu wa kabumbu, na ambao waliwahi kushiriakana nao na kumfanya ajihisi nyumbani katika enzi za maisha yake ya soka.
“Leo ni ya huzuni sana kwangu, leo ni siku ya kusema kwaheri kwa chochote nilichojitolea kufanya katika maisha yangu,” aliposti Silva.
“Leo pia ni siku ya kusema kwaheri kwa wenzangu, ambao ni kama familia kwangu. Nitawapeza sana na mzo wa shukrani kwa kuwa mlinifanya nijihisi nyumbani,” aliendela.
Mhispaniola huyo ambetambuliwa kuwa shujaa katika uga wa Etihad na vigogo wa ligi kuu Uingereza Man City, kwani aliisaidia klabu hiyo kujizolea mataji mbalimbali tangu alipojiunga nao 2010.
Kulingana na mwenyekiti wa Man City Khaldoon al-Mubarak, Silva ametambuliwa na atazidi kukumbukwa miongoni mwa wachezaji bora ambao wamewahi kuitumikia City, ambapo alijiunga na mashujaa wengine kama Vincent Kompany na Sergio Kun Aguero, na ambapo pia kuna mchongo wa picha yake ugani Etihad.
Mwanasoka huyo alisadia taifa lake la Uhispania kujinyakulia kombe la ulimwengu katika mashindano yaliyofanyika 2010, ikiwa pia alitangulia kunyakua taji la Euro 2008 na pia 2012 na timu yake asili.
Katika ligi kuu Uingereza, David Silva alishiriki mara 436 na ambapo aliisaidia klabu hiyo kujinyakulia mataji 11 muhimu, yakiwemo manne ya Premier, matano ya League Cup, mawili ya FA na matatu ya Community Shield.