PSG watishia kumtupa nje nahodha Marquinhos kwa tamko la hovyo kuhusu Mbappe

Miamba hao wa Ufaransa wanadai kuwa Marquinhos ameshindwa kuwa mfano kufuatia maoni yake na wanaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ni mali ya kupigwa mnada.

Muhtasari

• Wakati huo huo, Marquinhos amefichua kwamba anatumai Mbappe atasalia na timu hiyo msimu huu.

• Katika wito wa kutaka Mbappe abakie, Marquinhos anaamini kuwa mabingwa hao watetezi wa Ligue 1 ya Ufaransa bado wanahitaji wachezaji wao bora

PSG yakasirishwa na maoni ya Marquinhos kuhusu Mbappe.
PSG yakasirishwa na maoni ya Marquinhos kuhusu Mbappe.
Image: TWITTER

Ikiwa ni siku tano tu tangu nahodha na timu ya PSG, beki Marquinhos kufanya mahojiano ambapo alipata kuangazia sakata la Kylian Mbappe ambaye ametupwa nje ya timu hiyo kwa kukataa kusaini mkataba mpya, taarifa za ndani zinadai kwamba PSG hawakufurahishwa na mahojiano hayo na Marquinhos.

Tofauti na mshambuliaji Kylian Mbappé, mlinzi huyo wa Kibrazili alijumuishwa katika ziara ya klabu hiyo ya kabla ya msimu mpya barani Asia lakini aliwakasirisha wasimamizi wa klabu hiyo baada ya maoni yake, ambayo yalionekana kutoungwa mkono kabisa na msimamo wa klabu, katika mkutano na waandishi wa habari hivi majuzi.

Mbappé aliachwa nyumbani baada ya kusema kuwa hatasaini mkataba mpya Paris na, kwa kadiri klabu hiyo inavyoelewa, angemaliza mkataba wake kabla ya kuondoka kwenda Real Madrid msimu ujao wa bure jarida la Get Football.

Sports Brief Kenya pia wanaripoti kwamba Mbappe amekataa kurefusha mkataba wake na Parisians na pia amekataa kufanya mazungumzo na klabu ya Saudia Pro League Al-Hilal baada ya kuwasilisha ombi la rekodi ya dunia kwa fowadi huyo wa Ufaransa.

Miamba hao wa Ufaransa wanadai kuwa Marquinhos ameshindwa kuwa mfano kufuatia maoni yake na wanaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameshindwa kurejesha kiwango chake bora katika klabu hiyo tangu kuondoka kwa Thomas Tuchel mwaka 2020.

Wakati huo huo, Marquinhos amefichua kwamba anatumai Mbappe atasalia na timu hiyo msimu huu baada ya kuondolewa kwenye ziara ya kujiandaa na msimu mpya wa klabu hiyo nchini Japan, Goal inaripoti.

Katika wito wa kutaka Mbappe abakie, nahodha huyo wa PSG alisema kwamba anaamini kuwa mabingwa hao watetezi wa Ligue 1 ya Ufaransa bado wanahitaji wachezaji wao bora baada ya kuondoka kwa Lionel Messi msimu huu wa joto.