Jesse Lingard aanzisha klabu mpya kama mmilikiki baada ya kukosa nyota ya uchezaji

Aliichezea Nottinghma Forest mara 20 msimu uliopita, akifunga mabao mawili pekee. Kwa ujumla, aliichezea Man Utd mara 232, akishinda Kombe la FA na Ligi ya Europa akiwa na klabu hiyo.

Muhtasari

• Amekuwa akifanya mazoezi na Inter Miami na mchezaji mwenzake wa zamani wa United Ravel Morrison.

Jesse Lingard aanzisha klabu mpya
Jesse Lingard aanzisha klabu mpya
Image: INSTAGRAM

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Muingereza Jesse Lingard ametangaza kuanzisha klabu yake mpya ya soka baada ya kuachiliwa na Nottingham Forest msimu uliopita.

Kwa mujibu wa kituo cha habari za michezo cha BBC Sport, Lingard amethibitisha kuanzishwa kwa timu mpya inayobeba jina lake la utani, JLingz FC.

Lingard alitangaza mradi wake mpya na chapisho la Instagram, akiandika katika maelezo: "Timu mpya ya kandanda katika eneo la Manchester Kusini. Majaribio yatatangazwa hivi karibuni. JLINGZ FC HEART OF THE COMMUNITY."

Lingard bado anasaka klabu mpya ya kuendeleza soka lake baada ya kuondoka Nottingham Forest msimu huu wa joto. Amekuwa akifanya mazoezi na Inter Miami na mchezaji mwenzake wa zamani wa United Ravel Morrison huku akisubiri habari kuhusu uhamisho mwingine na amekuwa akihusishwa na DC United inayonolewa na Wayne Rooney, ingawa hakuna uhamisho ambao umefanyika hadi sasa, GOAL wanaripoti.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 atakuwa mwenyeji wa majaribio kwa JLingz FC na atazamia kusuluhisha mustakabali wake katika wiki na miezi ijayo.

Mashabiki walikuwa na furaha na timu nyingi za ndani ya Uingereza tayari ziko tayari kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya nyota huyo wa zamani wa West Ham.

Wakati huo huo, Lingard ameacha milango wazi ya kusaini klabu ya yoyote ya Saudi Arabia. Aliichezea Nottinghma Forest mara 20 msimu uliopita, akifunga mabao mawili pekee.

Kwa ujumla, aliichezea Man Utd mara 232, akishinda Kombe la FA na Ligi ya Europa akiwa na klabu hiyo.