Dirisha la Uhamisho la Ligi Kuu ya Uingereza hatimaye lilifungwa usiku wa kuamkia Jumamosi, Septemba 2 mwendo wa saa saba usiku.
Hii iliashiria mwisho wa ununuzi na ukopaji wa wachezaji kwa vilabu vya Uingereza baada ya miezi mitatu ya shughuli nyingi sokoni. Dirisha la uhamisho wa wachezaji litaendelea kufungwa hadi Januari 2024 ambapo vilabu vitaruhusiwa kununua au kukopa wachezaji.
Kumekuwa na miondoko mingi ya wachezaji ndani na nje ya vilabu katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Soko lilikuwa na shughuli nyingi zaidi siku ya mwisho ambapo vilabu kadhaa vilinunua wachezaji wapya, vingine vikachua wachezaji kwa mkopo au kuuza.
Hizi hapa ni baadhi ya dili zilizokamilika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho;-
- Rob Holding[Arsenal - Crystal Palace] £4m
- Sofyan Amrabat[Fiorentina - Manchester United] Mkopo
- Albert Sambi Lokonga[Arsenal - Luton] Mkopo
- Jonny Evans[Leicester - Manchester United] Huru
- Ryan Gravenberch[Bayern Munich - Liverpool] £34.3m
- Callum Hudson-Odoi[Chelsea - Nottingham Forest] Haijafichuliwa
- Sergio Reguilon[Tottenham - Manchester United] Mkopo
- Alex Iwobi[Everton - Fulham] £22m
- Andrew Omobamidele[Norwich - Nottingham Forest] £11m
- Divock Origi[AC Milan - Nottingham Forest] Loan
- Ibrahim Sangare[PSV Eindhoven - Nottingham Forest] Haijafichuliwa
- Luis Sinisterra[Leeds - Bournemouth] Mkopo
- Jaidon Anthony[Bournemouth - Leeds] Mkopo
- Jean-Ricner Bellegarde[Strasbourg - Wolves] Haijafichuliwa
- Neal Maupay[Everton - Brentford] Mkopo
- Mike Tresor[Genk - Burnley] Mkopo
- Brennan Johnson[Nottingham Forest - Tottenham] £45m+
- Odysseas Vlachodimos[Olympiakos - Nottingham Forest] Haijafichuliwa
- Nicolas Dominguez[Bologna - Nottingham Forest] Haijafichuliwa
- James McAtee[Manchester City - Sheffield United] Mkopo
- Ansu Fati[Barcelona - Brighton] Mkopo
- Clement Lenglet[Barcelona - Aston Villa] Mkopo
- Matheus Nunes[Wolves - Manchester City] £55m
- Nuno Tavares[Arsenal - Nottingham Forest] Mkopo
- Tommy Doyle[Manchester City - Wolves] Mkopo
- Cole Palmer[Manchester City - Chelsea] £40m
- Altay Bayindir[Fenerbahce - Manchester United] £4.3m
Kimataifa:
- Mason Greenwood[Manchester United - Getafe] Mkopo
- Joao Cancelo[Manchester City - Barcelona] Mkopo
- Remo Freuler[Nottingham Forest - Bologna] Mkopo
- Japhet Tanganga[Tottenham - Augsburg] Mkopo
- Marc Jurado [Manchester United - Espanyol] Haijafichuliwa
- Loic Mbe Soh[Nottingham Forest - Almere City] Mkopo