Lionel Messi na mimi tulipitia kuzimu huko Paris: Neymar atoa madai ya kustaajabisha

"...Alikwenda mbinguni na timu ya Argentina ilishinda kila kitu katika miaka ya hivi karibuni, na pamoja na Paris, aliishi kuzimu.” Neymar alisema.

Muhtasari

• Hata hivyo, zaidi ya misimu miwili, watatu hao waliweza tu kuondoka katika hatua ya 16 kabla ya Neymar na Messi kuondoka Paris majira ya joto.

Messi na Nyemar
Messi na Nyemar
Image: X

Mshambuliaji ghali kabisa katika ligi ya Saudi Arabia, Neymar ambaye hivi majuzi amesajiliwa AL Hilal kwa mara ya kwanza amefunguka makubwa jinsi mchezaji Lionel Mess ialiufanya wakati wake PSG kuwa mgumu baada ya kuhamia Ufaransa miaka miwili iliyopita.

Akishiriki tafakari yake juu ya msimu wake wa mwisho PSG, Neymar alifichua mawazo yake kwa chombo cha habari cha Brazil Globo, kama ilivyoripotiwa na Daily Post.

"Nilifurahi sana kwa mwaka aliokuwa nao, lakini wakati huo huo, huzuni sana kwa sababu aliishi pande zote za sarafu. Alikwenda mbinguni na timu ya Argentina ilishinda kila kitu katika miaka ya hivi karibuni, na pamoja na Paris, aliishi kuzimu.”

Lakini pia alikiri walishindwa "kuweka historia" nchini Ufaransa.

"Tuliishi kuzimu, yeye na mimi. Tunakasirika kwa sababu hatuko huko bure. Tuko hapo kufanya tuwezavyo, kuwa mabingwa, na kujaribu kutengeneza historia. Ndiyo maana tulianza kucheza pamoja tena; tulikutana pale ili tuweke historia. Kwa bahati mbaya, hatukufanikiwa."

Sports Brief wanaripoti kwamba baada ya Messi kujiunga PSG, Matarajio yalikuwa makubwa kwamba Neymar, Messi, na Kylian Mbappe wangeungana kuunda wachezaji watatu wa kutisha na kuiongoza PSG kupata mafanikio, haswa katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA.

Hata hivyo, zaidi ya misimu miwili, watatu hao waliweza tu kuondoka katika hatua ya 16 kabla ya Neymar na Messi kuondoka Paris majira ya joto.

Kutoweza kwao kuiongoza klabu hiyo kufikia utukufu wake ulioahidiwa kulifanya baadhi ya mashabiki wa PSG kuwaita 'mamluki' kutokana na mishahara yao mingi wakati huo.

Hata hivyo, wote wawili wamesonga mbele, huku Messi akishinda Kombe la Ligi kwa Inter Miami na kuiongoza klabu hiyo kufika fainali nyingine ya michuano ya US Open Cup.