Christiano Ronaldo awa mchezaji wa kwanza kuwahi kufunga mabao 850 rasmi

Siku ya Jumamosi, Ronaldo alifunga tena na kusaidia mabao mengine mawili katika ushindi wa 5-1 wa Al-Nassr dhidi ya Al-Hazem.

Muhtasari

• Kwa bao hilo, Ronaldo amefikia hatua ya kihistoria, kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya mchezo huo kufunga mabao 850 rasmi katika maisha yao ya soka.

Image: Instagram

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Christiano Ronaldo amekuwa mwanasoka wa kwanza kuwahi kutokea katika historia ambaye amefunga mabao 850.

Siku ya Jumamosi, Ronaldo alifunga tena na kusaidia mabao mengine mawili katika ushindi wa 5-1 wa Al-Nassr dhidi ya Al-Hazem.

Kwa bao hilo, Ronaldo amefikia hatua ya kihistoria, kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya mchezo huo kufunga mabao 850 rasmi katika maisha yao ya soka.

Sports Brief wanaripoti kwamba Bao hilo lilikuwa la sita katika mechi tatu zilizopita, na pia ametoa pasi nne za mabao katika kipindi hicho cha michezo mitatu. Kwa sasa anashikilia nafasi ya juu kwenye ligi kwa mabao na pasi za mabao.

Msimu wa kwanza wa Cristiano Ronaldo nchini Saudi Arabia haukufanyika kama ilivyotarajiwa.

Ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alifunga mabao mengi, alishindwa kupata kombe akiwa na Al-Nassr, matokeo ambayo si ya kawaida kwa mchezaji huyo maarufu wa Ureno.

Lakini msimu huu amekuwa na fomu nzuri ambapo ameisaidia Al-Nassr kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya Kiarabu kwa ushindi wa muda wa ziada dhidi ya Al-Hilal na kujihakikishia nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa ya AFC 2023-2024 kupitia ushindi wa ajabu wa kurejea katika raundi ya mchujo.

Ronaldo alicheza nafasi muhimu katika matukio yote mawili, haswa katika fainali ya Kombe, ambapo alifunga mara mbili.