Tazama orodha kamili ya wanasoka bora walioteuliwa kuwania Ballon d'Or

Iwapo Messi atashinda tena tuzo hiyo ya kifahari, itakuwa ni mara yake ya nane kuipeleka nyumbani.

Muhtasari

•Wanasoka mahiri walioteuliwa kuwania tuzo ya heshima zaidi katika soka, Ballon d’Or yalitangazwa siku ya Jumatano jioni.

•Lionel Messi, Erling Halaand na Kylian Mbapppe ni miongoni mwa wanaotajwa sana kushinda tuzo hiyo. 

Messi apokea tuzo la mchezaji bora kwa mara ya 7
Messi apokea tuzo la mchezaji bora kwa mara ya 7
Image: BALLON D'OR TWITTER

Majina ya wanasoka mahiri walioteuliwa kuwania tuzo ya heshima zaidi katika soka, Ballon d’Or yalitangazwa siku ya Jumatano jioni.

Jarida la France Football Magazine lilitangaza orodha ya wachezaji 30 walioteuliwa kuwania tuzo hiyo kabla ya hafla kuu ya tuzo itakayofanyika kwenye ukumbi wa Theatre Chatelet jijini Paris, Ufaransa mnamo Oktoba 30.

Mshindi wa Kombe la Dunia 2022 na Ligue 1 2022/23 Lionel Messi ni miongoni mwa wachezaji walioteuliwa. Katika orodha hiyo pia walikuwemo washambuliaji matata Kylian Mbappe wa PSG na timu ya taifa ya Ufaransa, Erling Halaand wa Manchester City na Norway, Mohammed Salah wa Liverpool na Misri, Bukayo Saka wa Arsenal na Uingereza, miongoni mwa wengine. Mshambulizi Christiano Ronaldo, ambaye sasa anachezea Al Nassr ya Saudi Arabia, hakufaulu kwenye orodha hiyo kwa mara ya kwanza tangu 2003.

Lionel Messi, Erling Halaand na Kylian Mbapppe ni miongoni mwa wanaotajwa sana kushinda tuzo hiyo. Iwapo Messi atashinda tena tuzo hiyo ya kifahari, itakuwa ni mara yake ya nane kuipeleka nyumbani.

Tazama orodha kamili ya wateuliwa  wa tuzo ya Ballon d'Or;

 

 1. André Onana - Manchester United/Cameroon
 2. Josko Gvardiol - Manchester City/Croatia
 3. Karim Benzema - Al Ittihad
 4. Jamal Musiala - Bayern Munich/Germany
 5. Mohamed Salah - Liverpool/Egypt
 6. Jude Bellingham - Real Madrid/England
 7. Bukayo Saka - Arsenal/England
 8. Randal Kolo Muani - Paris Saint-Germain/France
 9. Kevin De Bruyne - Manchester City/Belgium
 10. Bernardo Silva - Manchester City/Portugal
 11. Emiliano Martínez - Aston Villa/Argentina
 12. Khvicha Kvaratskhelia - Napoli/Georgia
 13. Rúben Dias - Manchester City/Portugal
 14. Nicolo Barella - Inter Milan/Italy
 15. Erling Haaland - Manchester City/Norway
 16. Yassine Bounou - Al Hilal/Morocco
 17. Martin Ødegaard - Arsenal/Norway
 18. Julián Álvarez - Manchester City/Argentina
 19. Ilkay Gündogan - Barcelona/Germany
 20. Vinícius Júnior - Real Madrid/Brazil
 21. Lionel Messi - Inter Miami/Argentina
 22. Rodri - Manchester City/Spain
 23. Lautaro Martínez - Inter Milan/Argentina
 24. Antoine Griezmann - Atletico Madrid/France
 25. Robert Lewandowski - Barcelona/Poland
 26. Kylian Mbappé - Paris Saint-Germain/France
 27. Kim Min-jae - Napoli/South Korea
 28. Victor Osimhen - Napoli/Nigeria
 29. Luka Modric - Real Madrid/Croatia
 30. Harry Kane - Bayern Munich/England