logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chelsea Legends: Terry amuomba Obi Mikel kurudi kutoka ustaafu, kujiunga ligi ya Saudia

Mikel Obi alikuwa mmoja wa wachezaji waliotia fora katika mechi ya wikendi.

image
na Radio Jambo

Habari12 September 2023 - 04:18

Muhtasari


• Kufuatia mechi hiyo, Terry alimtumia Mikel ujumbe kwenye mtandao wa Instagram akisema kuwa kiungo huyo wa kati wa Nigeria bado ana kipaji cha kuendelea kufanya vizuri.

John Obi Mikel

Aliyekuwa nahodha wa muda mrefu wa Chelsea John Terry amemtaka aliyekuwa mchezaji mwenza katika timu hiyo ya Uingereza John Obi Mikel kurudi kutoka ustaafu na kujiunga na ligi ya Saudi Arabia ili kucheza.

Terry alimwambia Mikel haya baada ya kuona mchezo wake wikendi wachezaji hao wa zamani wa Cheslea walipokuwa wakicheza na wenzao wa Bayern Munich.

Katika mechi hiyo ya malejendari, Chelsea walishinda mabao 4-0 huku Terry akifunga bao la pili kunako dakika ya 26 ambayo ilisadifiana na jezi yake ya muda mrefu – 26.

Mikel Obi alikuwa mmoja wa wachezaji waliotia fora na nahodha wa zamani wa The Blues John Terry anaamini kuwa Mnigeria huyo bado anaweza kufanya maajabu kwa kiwango cha juu.

Kufuatia mechi hiyo, Terry alimtumia Mikel ujumbe kwenye mtandao wa Instagram akisema kuwa kiungo huyo wa kati wa Nigeria bado ana kipaji cha kuendelea kufanya vizuri uwanjani.

“Mikel John Obi, bado unaweza cheza vizuri kaitka viwango vya juu vya soka, hebu kaa tayari kwa ajili ya kwenda Saudi Arabia,” John Terry alimwambia.

Mikel Obi alikuwa na mafanikio makubwa akiwa Chelsea, akishinda Ligi ya Premia mara mbili, Kombe la FA mara nne, Kombe la Ligi mara mbili, na Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved