Kocha Gareth Southgate amtetea Maguire baada ya bao la kujifunga, alaumu wanahabari

Southgate alisema kwamba hajawahi ona waandishi wa habari na mashabiki ambao wanachukia mchezaji raia wao kwa kwamba kitendo cha kila mtu kutupa lawama kwa Maguire kinachukiza sana.

Muhtasari

• Bao la kujifunga lilitokana na Maguire kujaribu kuchomoa krosi ya chini chini kutoka kwa nahodha wa Scotland Andy Robertson.

Harry Maguire na Gareth Southgate.
Harry Maguire na Gareth Southgate.
Image: X

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amemkingia kifua beki wa Manchester United, Harry Maguire, ambaye alijifunga katika mchezo wa kirafiki ugenini dhidi ya Scotland.

Maguire, aliyeanza mchezo kama mchezaji wa akiba kwa Uingereza katika ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Scotland, aliingizwa uwanjani wakati wa mapumziko kutokana na kuumia kwa Marc Guehi na alishangiliwa na mashabiki wa Scotland kwa kila pasi aliyopiga.

Katikati ya kipindi cha pili, aliweka mpira wavuni mwake. Hii ilifanya Scotland kurudi kwenye mchezo.

Bao la kujifunga lilitokana na Maguire kujaribu kuchomoa krosi ya chini chini kutoka kwa nahodha wa Scotland Andy Robertson, lakini kutokana na kukosa mawasiliano na kipa Aaron Ramsdale, mpira uliwekwa wavuni.

Bahati nzuri kwa Maguire, England walifanikiwa kufunga bao lingine lililofungwa na nahodha Harry Kane, ambalo liliifanya Three Lions kuwa kifua mbele 3-1 na kuuweka mchezo nje ya Scotland.

Kuondolewa kwa Kane kwenye mchezo muda mfupi baadaye kulimaanisha Maguire kufunga mchezo kama nahodha, katika muda ambao pengine ungerejesha kujiamini kwake baada ya makosa yake ya kujifunga.

Akimtetea Maguire ambaye alitupiwa maneno na wakosoaji, Southgate alisema;

"Sijawahi kujua mchezaji anayetendewa mabaya kama yeye. Amekuwa nguzo kabisa kwetu katika timu ya pili ya England yenye mafanikio kwa miongo kadhaa, amekuwa sehemu muhimu kabisa ya hilo.

"Kwa maoni ya mashabiki wa Scotland naipata. Lakini ni matokeo ya kumtendea ujinga kwa muda mrefu. Ni mzaha. Sio na mashabiki wa Scotland lakini na wachambuzi wetu wenyewe, wachambuzi au chochote kile.

 

Ramsdale naye alijitokeza kumuunga mkono Maguire, akisema baada ya mchezo kumalizika;

 

"Ninaweza kumuonea huruma kwa sababu nimekuwa upande mwingine wa Ligi Kuu nikipambana kusalia na nimeshuka daraja mara mbili. Yeye ni tishio kila wakati, anajua kuwa anaweza kulinda, anajua yeye ni kiongozi na napenda kucheza naye."

 

Maguire huenda akaonekana tena kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu watakapomenyana na Brighton kwenye Ligi ya Premia Jumamosi, Septemba 16.