Kikosi cha Brighton kilichopiga Man Utd nyumbani kiligharimu Euro milioni 16.2 tu!

Jumla ya kikosi hicho iliwagharimu euro milioni 16.2 tu kuichakaza Manchester United ambao walitumia mabilioni ya hela kuweka pamoja kikosi chao.

Muhtasari

• Kwa mujibu wa Sky Sports, Brighton walitumia kikosi cha bei ya chini kabisa kuidhalilisha United.

• Walidai kwamba kikosi hicho cha Brighton kiliwagharimu takribani euro milioni 16.2 pekee – sawa na shilingi za Kenya bilioni 2.95.

Brighton vs Man Utd
Brighton vs Man Utd
Image: X

Wikendi iliyopita timu ya Brighton iiidhalilisha Manchester United katika uga wa nyumbani – Old Trafford – kwa kibano cha mabao 3-1.

Katika mecho hiyo, kocha De Zerbi wa Brighton alichezesha kile kinachoweza kuitwa kikosi chake hafifu kabisa baada ya kuwapumzisha wachezaji 6 wa kikosi cha kwanza.

Sasa shirika la habari la Sky News limebaini kwamba kikosi amabcho kilicheza dhidi ya United kilikuwa kimejaa wachezaji limbukeni.

Kwa mujibu wa Sky Sports, Brighton walitumia kikosi cha bei ya chini kabisa kuidhalilisha United.

Walidai kwamba kikosi hicho cha Brighton kiliwagharimu takribani euro milioni 16.2 pekee – sawa na shilingi za Kenya bilioni 2.95.

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 34, Man Utd wamepoteza mechi tatu kati ya tano za kwanza za ligi msimu mmoja, huku kipigo hicho cha Old Trafford kikimaliza msururu wa michezo 20 bila kufungwa nyumbani kwenye Premier League.

Baada ya kuuza wachezaji muhimu katika msimu wa majira ya Joto, wengi walidhani ndio mwanzo wa mwisho kwa Brighton lakini wameendelea kufana wakitumia wachezaji limbukeni kabisa.

Mlinda lango Steele hakuwagharimu chochote na aliweza kuiziba vilivyo nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Robert Sanchez akitimukia Chelsea.

Katika safu yao ya nyuma, beki Lewis Dunk walimpata bure, huku wakitumia kima cha euro milioni 1.5 kumnasa Lamptey, euro milioni 1.7 kumnasa Van Hecke na laki 9 kumnasa Veltman beki wa kulia,

Safu ya kati walitumia kima cha euro milioni 2.6 kumnasa Gross huku Dahoud wakimpata kwa bei ya sare.

Brighton
Brighton

Katika safu matata ya ushambulizi kwa kikosi kilichocheza dhidi ya United, Dan Welbeck walimpata kwa sare, Mitoma wakimnasa kwa euro milioni 2.6, Adingra wakimpata kwa euro milioni 6.8 na Lallana wakimpata kwa sare.

Jumla ya kikosi hicho iliwagharimu euro milioni 16.2 tu kuichakaza Manchester United ambao walitumia mabilioni ya hela kuweka pamoja kikosi chao.