Je, ni kweli wachezaji wa Man Utd walipigana wenyewe baada ya kupigwa na Brighton?

Baada ya kufunzwa soka nyumbani na cijana wa timu ya Brighton mbele ya mashabiki wa Old Trafford, inaarifiwa wachezaji wa United waliangushiana hasira wenyewe kwa wenyewe, wachezaji 4 walihusika.

Muhtasari

• The Sun sasa wamedai kuwa baada ya kushindwa hivi karibuni, nyota wanne walihusika kwenye mpapurano katika chumba cha kubadilishia nguo.

Wachezaji wa Man Utd
Wachezaji wa Man Utd
Image: X

Kufuatia kipigo cha Brighton nyumbani Old Trafford wikendi iliyopita, kuliibuka tetesi kwamba wachezaji wa Manchester United walipigana wenyewe katika chumba cha kubadilisha nguo wakitupiana lawama kufuatia kipigo hicho.

Lakini sasa taarifa mpya ni kwamba uongozi wa timu hiyo umejitokeza na kukanusha vikali tetesi hizo kwa kusema kwamba hakuna tukio lolote la vita lililotokea katika chumba chao cha kubadilisha nguo baada ya kukamilika kwa mechi hiyo.

The Red Devils waliendelea na msimu wao wa misukosuko ambao umekumbwa na matatizo ndani na nje ya uwanja - huku Erik ten Hag akiwa tayari amehusika katika ugomvi na Jadon Sancho kuhusu uchezaji wake wa mazoezini.

Kampeni hiyo pia imeshuhudia kutoridhishwa na mashabiki kutokana na kushindwa kwa Glazers kuiuza klabu hiyo huku mazungumzo ya kutwaa klabu hiyo yakiendelea, huku hali ya sumu ikionekana kuathiri wachezaji baada ya kushindwa mara tatu katika mechi zao tano za kwanza.

The Sun sasa wamedai kuwa baada ya kushindwa hivi karibuni, nyota wanne walihusika kwenye mpapurano katika chumba cha kubadilishia nguo.

Ripoti hiyo inadai kuwa nahodha Bruno Fernandes alikuwa mmoja wa nyota wa hadhi ya juu waliohusika baada ya kukabiliana na mchezaji mwenza Scott McTominay.

Mabeki Lisandro Martinez na Victor Lindelof - ambao wote walicheza kwa pamoja kwa dakika 90 - pia inasemekana 'wamepotezana', huku meneja Ten Hag 'akijaribu kurejesha utulivu' huku uchunguzi wa baada ya mechi ukianza.

Hata hivyo, Manchester United ilikanusha madai ya ripoti hiyo ilipowasiliana na Mail Sport.