Man City yabanduliwa Carabao Chelsea wakifunga bao lao la kwanza mwezi Septemba

Ilikuwa ni mara ya pili kwa Jackson kufunga tangu alipowasili majira ya joto ya pauni milioni 32 kutoka Villarreal, baada ya kushinda 3-0 katika mechi ya ligi dhidi ya Luton Town mwezi uliopita.

Muhtasari

• Jackson pia alikuwa na bao la pili ambalo kwa utata lilikataliwa kuwa nje ya kuotea jambo ambalo lingeongeza uongozi wa timu yake mara mbili.

Chelsea.
Chelsea.
Image: Chelsea

Hatimaye timu ya Chelsea imekata kiu ya mabao baada ya kufunga bao lao la kwanza kabisa tangu mwezi Septemba kuanza huku zikiwa zimesalia siku 2 tu kuelekea mwisho wa mwezi huu.

Hata hivyo, Chelsea watamaliza mwezi huu bila kuwa na bao lolote kwenye michezo yote ya ligi kuu ya premia kwani bao hilo lao lililofungwa na mshambuliaji wao Nicolas Jackson lilikuwa ni katika mchezo wa Carabao Jumatano usiku dhidi ya Brighton.

Jackson aliwapa matumaini ya kusonga kwenye hatua nyingine baada ya kuvurunda katika mechi kadhaa za premia kwa kukosa nafasi za wazi mbele ya lango, kile ambacho kocha wake Mauricio Pouchettino alikitaja kama kutojiamini anapofika mbele ya lango.

Ilikuwa ni mara yake ya pili kufunga tangu alipowasili majira ya joto ya pauni milioni 32 kutoka Villarreal, baada ya kushinda 3-0 katika mechi ya ligi dhidi ya Luton Town mwezi uliopita.

Jackson pia alikuwa na bao la pili ambalo kwa utata lilikataliwa kuwa nje ya kuotea jambo ambalo lingeongeza uongozi wa timu yake mara mbili zikiwa zimesalia chini ya dakika 20. Huku VAR ikiwa haijatumika hadi nusu fainali ya shindano hilo, uamuzi wa uwanjani ulisimama.

Kwingine, mabingwa watetezi wa ligi ya premia Manchester City walibanduliwa nje ya Carabao na Newcastle United kwa bao moja komboa ufe.

Newcastle sasa watamenyama katika hatua ya 16 bora na mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester United.

Chelsea watacheza dhidi ya Blackburn Rovers katika hatua ijayo ya Carabao.