Obi Mikel atabiri klabu pekee cha Uingereza ambacho kitampa ufanisi Victor Osimhen

Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea anasema anatumai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 atahamia klabu hiyo ya Stamford Bridge licha ya Manchester United kumtaka.

Muhtasari

• “Hicho ndicho wanachokitafuta; mshambuliaji anayetaka kukimbia nyuma ya mabeki kwa sababu anaisaidia timu."

Obi Mikel amtaka Osimhen kuingia Chelsea
Obi Mikel amtaka Osimhen kuingia Chelsea
Image: Insta

Kiungo mkabaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Super Eagles ya Nigeria John Obi Mikel amemtaka mshambuliaji wa Nigeria na timu ya Napoli, Victor Osimhen kufanya uamuzi wa kujiunga na Chelsea endapo ataondoka Napoli Januari.

Uhusiano wa Osimhen na Napoli umeonekana kuingia doa katika siku za hivi karibuni baada ya akaunti ya TikTok ya klabu hiyo kupakia video iliyochukuliwa kuwa na kumdhihaki Osimhen baada ya kukosa kufunga mkwaju wa penati siku chache zilizopita.

Kufuatia uhusiano huo kuingiwa doa, wengi wanahisi kwamba straika huyo matata huenda ataondoka Italia katika dirisha dogo la uhamisho mwezi Januari na Obi Mikel kupitia kwenye Podasti yake amemtaka Osimhen kufanya uamuzi wa busara kujiunga na Chelsea kwani ndio timu pekee nchini UIngereza ambayo itampa ufanisi ambao angepedna kujilimbikizia.

Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea anasema anatumai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 atahamia klabu hiyo ya Stamford Bridge licha ya Manchester United kumtaka.

Kulikuwa na wasiwasi kwamba mshambuliaji huyo anaweza kutafuta njia yake ya kutoka licha ya kuwaongoza kutwaa ubingwa wa Serie A msimu uliopita.

Na Mikel amesema kuwa Osimhen atamudu EPL. Nyota huyo wa zamani wa Stoke City aliiambia Obione Podcast:

"Nadhani ninapomtazama miaka michache iliyopita, lakini sasa, nikimtazama msimu uliopita na kumtazama msimu huu, ningesema kwa hakika. Angeingia kwenye Ligi Kuu na kuingia moja kwa moja. Atakufungia mabao, atakimbia nyuma ya mabeki, atanyoosha timu na nadhani hiyo ndiyo timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu sasa.

“Hicho ndicho wanachokitafuta; mshambuliaji anayetaka kukimbia nyuma ya mabeki kwa sababu anaisaidia timu.

"Kwa sababu inawanyoosha mabeki, natumai anakuja Chelsea. Lakini kutokana na kelele ninazosikia, nadhani yeye ni United kubwa, nadhani pengine.”