Video ya mchezaji nguli wa Al Nassr na timu ya taifa ya Senegal, Sadio Mane na wenzake wakifurahia kukwepa timu yao kuwekwa kwenye kundi moja na Nigeria kwenye michuano ya AFCON Januari mwakani nchini Ivory Coast imewapa Wanaijeria kila sababu ya kutamba kuwa wanaogopwa.
Droo hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Parc des Expositions d'Abidjan nchini Ivory Coast, huku magwiji kadhaa wa soka barani Afrika wakihudhuria.
Nyota huyo wa zamani wa Liverpool alikuwa sehemu ya wasaidizi waliotoa droo katika mchezo huo, huku akisaidia kukamilisha droo hiyo pamoja na beki wa Paris Saint-Germain Achraf Hakimi, magwiji wa Chelsea Didier Drogba na John Mikel Obi.
Nigeria ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji, Ivory Coast, na Equatorial Guinea na Guinea-Bissau, kulingana na Soccernet.
Baada ya Wasenegali kusikia kuwa hawatokutana na Nigeria kwenye hatua ya makundi, walipasa kelele za furaha wakiongozwa na Mane mwenyewe.
Mabingwa watetezi wanaweza kuwaepuka Super Eagles kwenye sare hiyo, lakini walipata taifa lingine bora katika historia ya shindano hilo, ambalo ni Cameroon.
Katika kundi lao mbali na Cameroon, Senegali pia watakutana na Gambia na Guinea.
Lions of Teranga wa Senegal watakuwa wakihaha kutetea ubingwa wao wa AFCON katika taifa hilo la Afrika Magharibi lakini watakabiliana na timu ya Indomitable Lions ya Cameroon ambao walipangwa nao katika Kundi C.